POLICARP Kardinali Pengo.
MUFTI Simba.
Kama nilivyoanza kujiuliza hapo juu. Ni kwa nini viongozi wa kisiasa hualikwa kwenye matukio ya kidini. Kuna sababu gani kumualika kiongozi wa kisiasa kwenye shughuli za Kiimani/ Kiroho? Je ni kujikomba/kujipendekeza kwa viongozi wa dini kwa viongozi wa kisiasa au kinyume chake? Je kumualika/kumleta kiongozi wa kisiasa katika shughuli ya kiroho kuna msaada wowote kwa waumini kiroho? Nijuavyo mwanasiasa siku zote/popote uhubiri siasa. Sasa kumleta/kumualika Kiongozi wa kisiasa kwenye matukio ya kiroho huwa viongozi hawa wa dini hutaraji nini toka kwa wanasiasa? Kuna sababu gani kila uapisho wa Mchungaji,Askofu hata wa 'tudhehebu twa kibiashara' Sherehe za Maulidi, kila Idd,kuwaalika viongozi wa Kisiasa? Hivi na nchi za wenzetu mambo yako hivi? Binafsi inanikanganya sana. Kwenu Wadau.
(Wenu mdau mdadisi Wa Mambo, mkitaka jina nitawatajia)
No comments:
Post a Comment