Thursday, June 02, 2011

MKANGANYIKO leo; Maswali matatu ya Lowassa kwa Msekwa.



Gazeti la Mwanahalisi la leo June 1. 2011 limenukuu yaliyojiri katika kikao kinachoelezwa kufanyika katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kati ya viongozi wakuu wa CCM, Katibu Mkuu Wilson Mukama na  Makamu Mwenyekiti Pius Msekwa. Kikao kilichowahusisha Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge. Yote katika yote yaliyoandikwa kuwa yalijiri katika kikao hicho kubwa zaidi ni maelezo ya majibizano kati ya Lowasa na Pius Msekwa. Na zaidi maswali matatu ya Lowasa kwa Msekwa. Majibizano hayo yalikuwa hivi. Msekwa...."Lowasa unatakiwa kujiuzulu nyadhifa zako zote kwenye chama ili kutekeleza maagizo ya NEC na falsafa ya kujivua gamba". 
Imeelezwa kuwa Lowasa alijieleza kirefu juu ya namna asivyohusika na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond na namna alivyofanya tukio la kizalendo kwa maslahi ya Taifa na chama, Tukio la kujiuzulu uwaziri mkuu na alivyokutana na Rais hivi karibuni. Baada ya maelezo marefu ya Lowasa, Msekwa alisema... "Lowasa Acha mbio zako za Urais". Lowasa akajibu kwa upole. "Lini nimetangaza kugombea urais"? Akaongeza swali, "Lakini hata kama ninataka kufanya hivyo ni haramu kugombea nafasi hiyo?, Je kuna mliyemuandaa?" Maswali haya matatu ya Lowasa kwa Msekwa yananikanganya sana. Mdau nini tafakari yako juu ya maswali haya na hali halisi ya kisiasa ya CCM?

No comments:

Post a Comment