Ndugu zangu,
AFRIKA kuna mambo. Na Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia. Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa!
Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi. Lakini mie ni mmoja kati ya wachache, ambao, kwenye pambano kama hilo, hupenda kusimama katikati, hata kama ni kazi ngumu.
Na punde tu imemalizika raundi ya kwanza ya mpambano wa majogoo; Freeman Vs Police. Ndio, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa kambi ya Upinzani ameachiwa huru leo kule Arusha baada ya kujisalimisha polisi juzi na kisha kulazwa rumande. Na tumesikia, kule Arusha amesafirishwa kwa ndege!
Kimsingi, Freeman alichemka kwa kutokuwa makini na kufuAtilia taratibu za Mahakama. Kama mwenyekiti wa Chama na Kiongozi wa kambi ya Upinzani alitakiwa awe mfano katika umakini. Lakini, Polisi walichemka zaidi kwa kumkamata Freeman aliyekwenda mwenyewe kituoni kujisalimisha na hata kumlazimisha avue viatu na kumsweka rumande.
Hivi, kulikuwa na lazima ya polisi kutumia rasilimali zote zile kwa mtu mmoja Freeman Mbowe? Ni kiasi gani haswa kimetumika kugharamia ’operesheni’ ile ya kumfikisha Freeman mahakamani Arusha? Freeman Mbowe hafanani hata kidogo na Mulla Omar!
Kwa kilichofanyika , Freeman Mbowe na Chadema yake walijikuta wakipigiwa penalti mikononi. Ningalikuwa afande wa polisi ningeelekeza moja tu; Kama Freeman kajisalimisha, aambiwe vema na aamrishwe kurudi kituoni alfajiri siku inayofuata tayari kwa safari ya Arusha akiongozana na polisi wa kiraia. Safari hiyo iwe ya kipolisi na wala asisindikizwe na viongozi wa Chadema wala mashabiki wake.
Na sharti ni moja tu; asipoonekana kituoni kumi na mbili alfajiri, basi, akamatwe na kusafirishwa akiwa na pingu mikononi. Makubaliano hayo yatiwe saini na Freeman mwenyewe.
Hivyo basi, kiungwana, Freeman angeambiwa arudi nyumbani kwake, akaungane na familia yake. Awaage kwa amani kuwa kesho yake ana safari ya kwenda Arusha akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa kiraia. Juu ya yote, Freeman ni mheshimiwa mbunge, na kiongozi wa kambi ya upinzani, anastahili hata kuwa na body guard anayelipwa fedha za walipa kodi.
Hatua hiyo ya kiungwana ya polisi ingebakisha pigo kwa Freeman, maana, focus ingebaki kwenye uzembe wake mwenyewe ( Freeman) wa kutofuatilia kwa makini taratibu za kimahakama.
Badala yake, kitendo kile cha polisi kumweka rumande Freeman na kumsafirisha kwenda Arusha katika mazingira tuliyoyaona kimehamisha focus ya tatizo la msingi la Freeman, uzembe. Kimeipa Chadema sympathy ya umma kwa dhana ile ile, kuwa wanaonewa. Na juu ya hapo Chadema inanunua umaarufu kwa gharama nafuu. Na siasa inahusu kutafuta umaarufu kwa wapiga kura. Ukifanikiwa kumwonyesha mwingine si makini, basi, unampunguzia umaarufu.
Si tumeona, sasa Freeman anaonekana ’ shujaa’. Tena kamanda ngangari, si amelala hata rumande! Afrika U-Mandela ni sifa ya ziada kwenye CV ya mwanasiasa. Na mahabusu za Afrika zinatofautiana. Watu wanajua, kuwa mahabusu wengine hutayarishiwa ’ makao’ yao, iwe Keko au Ukonga.
Si tulisikia habari za Keko kufanyiwa ukarabati kuandaa ’ makao’ ya akina Grey Mgonja na Basil Mramba . Naam. Mahabusu wengine ni ’ Waheshimiwa’. Hata Keko wanalala kwenye viyoyozi na kuangalia runinga bila kubughudhiwa na mahabusu wengine. Na hapa ndipo wengine wanaziona chembe za uonevu.
Na katika hili la Freeman na polisi limemwibua hata Profesa Ibrahim Lipumba aliyepotea kwenye ’ game’. Ndio, Lipumba kwa kipindi kirefu sasa amepotea uwanjani. Ghafla, naye ameiona krosi hii iliyopigwa na Chadema baada ya kuudaka kirahisi mpira wa penalti.
Ndio, Profesa amerudi tena uwanjani. Ameishutumu vikali polisi na kutamka kuungana na Chadema kwenye kuandama. Na media imempa Profesa coverage ya kutosha. Wako wapi sasa wanaosema CUF ni CCM ’ B’? Profesa ni mzoefu kwenye mchezo wa siasa.
Lakini, kuna mchezaji kwenye timu ya upinzani ambaye hata kwenye jukwaa la watazamaji haonekani siku hizi. Si Unamjua? Au labda nikusaidie; Ni James. Alipata kuwa mshambuliaji hatari sana. Lakini sasa hata kivuli chake hakionekani. Ni James Mbatia wa NCCR.
Kulikoni NCCR? Au inahusu ugomvi wa jimbo la Kawe na madai ya bilioni moja kwa Chadema? Lakini hata Profesa si ana kaugomvi na Chadema, lakini, kwa penalti ile ya Polisi kuwapigia Chadema mikononi, Profesa ameamua kusahau ya nyuma na kurudi kwenye ’ game’.
Na swali ni hili; Je, Profesa naye amerudi|? Au ni shambulizi la msimu tu?
Na tusubiri tuone.
Maggid,
Iringa,

No comments:
Post a Comment