MDEGELA akijieleza kwa waumini wake wa KKKT Iringa Mjini (pichani chini) huku wao wakimsikiliza kwa makini.
Msaidizi wa Mdegela Mch. Blaston Gavile akisikiliza maelezo ya Askofu wake.
Akiendelea kueleza.
ASKOFU wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Iringa Dkt Owderburg Mdegella (pichani ) atangaza kulisamehe bure gazeti la Mwana Halisi na kuwa baadhi ya maaskofu wenzakwe ,wachungaji na waumini wake wake wanamhujumu .
Askofu Dkt Mdegella aliyasema hayo leo mbele ya waumini wa kanisa kuu wakati akitoa tamko la Halmashauri kuu ya dayosisi ya Iringa iliyokutana juzi mjini Iringa kwa ajili ya kuchunguza na kutolea uamuzi wa mwisho dhidi ya tuhuma mbali mbali zilizotolewa na gazeti la Mwana Halisi na baadhi ya mitandao na kuelekezwa kwa askofu huyo.
katika tuhuma hizo zilizotolewa na gazeti la Mwanahalisi toleo namba 243 ikiwa na kichwa cha habari kisemacho Askofu wa KKKT katika tuhuma nzito gazeti hilo lilidai kuwa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa, limetumbukia katika mgogoro mzito na wa aina yake ambao, iwapo busara haitatumika utaweza kuliacha kanisa limekatika vipande viwili, imefahamika.

Habari hizo ambazo zimetapakaa na hata kuifikia ikulu ya Rais Jakaya Kikwete, vyombo vya habari, polisi na idara ya usalama wa taifa, zinamtuhumu mkuu wa kanisa hilo, Askofu Owdenberg Mdegella kwa ufisadi.
Madai dhidi ya askofu yameorodheshwa katika andishi lenye maneno 2008 lililopelekwa kwa maaskofu wote wa KKKT, ikulu, taasisi (mbalimbali) na vyombo vya habari. Lilisambazwa kwa njia ya baruapepe.
DKt Mdegella alisemas kuwa mchezo mchafu unaofanywa na maaskofu wachache na wachungaji pamoja na waumini wa kanisa hilo na makanisa mengine kwa ajili ya kutaka kuivuruga Dayosisi ya Iringa tuhuma ambazo hazina ukweli wowote na kuwaomba waumini kuzipuuzia tuhuma hizo.
Alisema kuwa mkutano wa Halmashauri kuu ya wachungaji umepuuza taarifa za upotoshwaji zinazotolewa na kuwa uchunguzi na usaliti unaofanywa na kikundi hicho umepuuzwa na kuwa hauna maana yeyote ndani ya kanisa hilo.
Hata hivyo alisema kuwa maamuzi yote dhidi ya uchunguzi na maamuzi ya Halmashauri kuu yatafikishwa kwa mkuu wa kanisa hilo na wajumbe wa Halmashauri kuu na maazskofu wale wachache.
Alisema kuwa hajaona ni vema maamuzi hayo kutolewa mbele ya waumini wote na kuwa kufanya hivyo ni kulivuruga kanisa iwapo mambo mabaya yatatolewa madhabahuni ambako si mahali pake.
'' Kwa hiyo ninyi wakristo nasema hivi yapuuzeni mambo yote mabaya yanayotolewa na wale wasiolitakia kanisa mambo mema na mimi kama askofu wenu ambaye nimechafuliwa napenda kutangaza mbele yenu kuwa nawasamehe wote waliohusika katika mpango wa kunichafua katika gazeti hilo na mitandao pia nawasamehe wale wote waliohusika kufurahia habari hiyo ya uchochezi na mwandishi wa habari hiyo''
No comments:
Post a Comment