Wabunge wa Chadema Warudi Tanzania baada ya Ziara Nchini Marekani
Waheshimiwa
wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamerejea Tanzania
Baada ya ziara ya Wiki moja nchini Marekani ambapo walikwenda kufungua
Tawi la Chadema Washington DC. Mbali na kufungua Tawi wabunge hao pia
walibahatika kukutana na baadhi ya Watanzania waishio Marekani na
kubadilishana nao mawazo mbalimbali kuhusiana na Mustakabali wa Taifa
letu. Pia walibahatika kutembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani na kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi
Maajar. Wakiongelea ziara hiyo Wabunge hao walisema ilikuwa na mafanikio
makubwa kwani wamejifunza mambo mbalimbali. Wabunge hao wamewashukuru
sana Watanzania wote waishio Washington DC waliojitokeza siku ya
ufunguzi wa Tawi la Chadema na Pia wamewashukuru Uongozi wa Tawi la
Chadema Washington DC kwa Ukarimu walioonyesha katika kipindi chote
walipokuwa Washington DC.
No comments:
Post a Comment