JK Mazoezini
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha,
akiwa katika mazoezi yake ya kutembea kilomita tatu kila asubuhi na
jioni kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka
mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha
ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua
hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kujenga afya
kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga
mfano wake(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment