KAMPUNI
ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania
imewatahadharisha wateja wao wa huduma ya M-pesa kuwa makini kulinda
namba zao za siri zisifahamike na watu wengine, kuepuka kuibiwa fedha
zao.
Akizungunza
na waandishi wa habari juzi ofisini kwake Mlimani city Jijini Dar es
salaam, afisa mawasiliano na mahusiano Joseline Kamuhanda ameelezea
madhara yatokanayo na kuvuja kwa namba za siri za mteja, hali
inayosababisha wizi.
“Ukweli
mteja akitoa namba ya siri kwa wakala ili amsaidie kumtolea pesa
katika akaunti yake ni hatari, kwa vile itategemea wakala huyo atakuwa
na uadilifu wa kiasi gani, lakini pia hata kwa mtu wa karibu kumpa
kufahamu namba ya siri si jambo jema “ alisema Kamuhanda.
Akizungunzia
kuboreshwa kwa mtandao huo alisema M-pesa imezidi kuimarika baada ya
kuondoa tatizo la ‘network’ kusumbua wakati Fulani, hali ambayo ilileta
malalamiko kwa wateja.
“Tatizo
la mtandao kusumbua katika zoezi utumaji pesa na upokeaji halipo baada
ya wataalam kulifanyia kazi kikamilifu na kuliondoa” alisema Kamuhanda.
Akisisitiza
kuhusiana na huduma za M-pesa afisa mkuu wa biashara Dylan Lennox
amewaomba wateja kuwa na utamaduni wa kutuza namba za siri ikibidi
kuzibadilisha kila baada ya muda, kuzuia hata ndugu wa karibu au rafiki
kuikariri namba hiyo.
“Kuna
watu wapelelezi wa mambo anakuzoea inafikia kujua namba ya siri ya
akaunti yako, siku unataka kutioa fedha katika akaunti yako unaambiwa
huna fedha za kutosha, badala yake unalaumu Vodacom wamekuibia kitu
ambacho si kweli” alisema Lennox.
Alisema
tatizo la mteja kuibiwa linahusiana na yeye mwenyewe kutoficha namba ya
siri pengine kwa kutofahamu vyema namna ya njia za utoaji fedha kwa
njia ya M-pesa, bila kujua huyo aliyempa namba ya siri ameikalili na
kutumia kumuibia.
Na Zainul Mzinge
No comments:
Post a Comment