Mbunge wa Singida Mashariki na Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu akionyesha shati lake alilodai kuchaniwa na polisi baada ya kumpa kichapo akiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara baada ya kupata dhamana jana. Picha na Anthony Mayunga
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, na wenzake saba ambao juzi walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kusomewa mashtaka matatu ya kuingia eneo la hospitali bila kibali, kufanya mkutano na kuzuia watu kufanya kazi, wamepata dhamana lakini wamezuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo hadi kesi inayowakabili itakapokwisha.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Yusto Roboroga alitoa uamuzi huo akisema ni kwa mujibu wa kifungu cha Sheria Namba 148 cha Makosa ya Jinai, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambacho kinatoa haki kwa watuhumiwa kupata dhamana. Alitoa uamuzi huo baada ya kupitia pingamizi lililowekwa na upande wa mashtaka kutaka wasipewe dhamana. Hata hivyo, alisema: “Washtakiwa wanazuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo mpaka kesi hiyo itakapokuwa imekwisha."
Hakimu huyo alisema kwa kuwa washtakiwa hao ni viongozi wakubwa wa chama walizuiwa ili kupunguza shinikizo la wanachama kutokana na tukio lililojitokeza, lakini kwa kuwa mazishi yameshafanyika, alisema wanaweza kudhaminiwa kama watakidhi masharti.
Hakimu Ruboroga alitaja masharti ya dhamana hiyo kuwa ni kusaini mkataba wa dhamana wa Sh5 milioni kwa wadhamini wawili wanaoaminika.
Kwa wasio wakazi wa Tarime, alisema watatakiwa kupeleka mahakamani hati za mali isiyohamishika. Washtakiwa wote walikidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana hadi Juni 26, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Juzi, Lissu na wenzake, Waitara Mwita Mwikwabe, Stanslaus Nyembea, Anderson Deogratias Chacha, Andrew Andalu Nyandu, Mwita Marwa Maswi, Bashiri Abdalllah Selemani na Ibrahimu Juma Kimu walifikishwa mbele ya mahakama hiyo na kusomewa mashtaka hayo matatu na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Casmir Kiria ambaye alisema, waliyatenda Mei 23, majira ya saa nne usiku. Wote walikana mashtaka hayo.
Maiti wazikwa, wananchi wataka kurejesha majeneza polisi
Hatimaye maiti wote waliokuwa wametelekezwa barabarani wamezikwa na ndugu zao huku baadhi ya familia zikikataa kuwazika kwa majeneza ya polisi na kutumia yale yaliyokuwa yameandaliwa huku wengine wakipanga kuyarudisha kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime, Constantine Massawe.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kewanja, Om’tima Tanzania alisema kuwa mmoja wa marehemu hao, Chacha Ngoka alizikwa na jamii. Hata hivyo, alisema polisi waliweka mwili wake ndani ya jeneza bila kuweka sanda hali ambayo iliwalazimu kumweka ndani ya jeneza lao na kumvika sanda. Hilo lilifanyika pia katika eneo la Nyakunguru alikozikwa marehemu Emmanuel Magige.
Katika Kijiji cha Bonchugu, Serengeti, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Mwikwabe Makena alidai kwamba walilazimika kuzika mwili wa marehemu Chawali Bhoke uliotelekezwa na polisi.
Alidai kwamba kabla ya kuutelekeza, walifyatua mabomu ya machozi na risasi hewani baada ya wananchi waliokuwa wamebeba pinde, mishale, mikuki na mapanga kujaribu kuzuia gari la polisi. Alisema walilazimika kuzika bila kuwapo kwa ndugu wa marehemu waliokuwa wameachwa Tarime.Hata hivyo, Kamanda Massawe na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz hakuwa tayari kuzungumzia madai hayo.
Wataka RC, DC wawajibishwe
Baadhi ya wananchi wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Enos Mfuru, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewelle na Kamanda Massawe kwa madai ya kushindwa kudhibiti uvunjifu wa amani.
Walisema viongozi hao wamekuwa wakijaribu kuficha ukweli wa kilichotokea katika mauaji hayo ya watu watano na kujeruhi wengine 10 na kusababisha kuvunjika kwa amani.
Mmoja wa wananchi hao, Marwa Sasi alisema kitendo cha polisi kufanya mauaji hayo na kuchukua maiti hospitali na kuzitelekeza njiani hakistahili kuachwa kipite hivihivi bila hatua kali za kinidhamu kuchukuliwa.
“Ukweli ni kwamba vijana wameuawa na kujeruhiwa. Tatizo ni nini litafutwe, si kudanganya umma mara walikuwa 800, 1,000 au 1,500, majambazi, wavamizi, walikuwa na silaha mbona tunaona majeruhi na maiti hatuoni askari waliojeruhiwa?”
Bavicha lakusudia kuandamana
Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Dar es Salaam limesema liko tayari kuandamana hadi magerezani kudai haki itendeke baada ya kutokea kwa mauaji katika tukio la uvamizi wa Mgodi wa Nyamongo.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo alisema kitendo hicho ni kinyume cha haki za binadamu. “Kitendo kilichofanywa na polisi cha kuwaua raia ni cha kulaaniwa na kupigwa vita ili kisijirudie tena kwa kuwa vitendo hivyo vinafanywa kwa maslahi ya wachache,” alisema.
Kilewo alisema kuwa chama hicho kitahakikisha haki inatendeka na kusisitiza kwamba kipo nyuma ya wananchi ambao ndugu zao wamefariki kutokana na tukio hilo... “Tutahakikisha kuwa Mtanzania anaheshimiwa katika taifa lake. Mauaji kama hayo yalitokea Arusha, sasa wameua tena Tarime... Hatuwezi kuvumilia kamwe.”
Wana Kawe nao wazungumzia mauaji Tarime
Kundi la watu waliodai kuwa wanawawakilisha wakazi wa Jimbo la Kawe wamewataka Mawaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Nishati na Madini, kujiuzulu kwa kushindwa kuzuia mauaji ya wananchi yanayotokea mara kwa mara kwenye migodi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kiongozi wa kundi hilo, Powell Mfinanga alisema kutokana na matukio ambayo yanahusisha wananchi wasio kuwa na hatia, umefika wakati wa viongozi hao kuwajibika.
“Inaonyesha kabisa wizara hizi zimeshindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na kuibuka kwa migogoro ya mara kwa mara kati ya wawekezaji wa madini na wananchi hali inayosababisha raia kupoteza maisha yao,” alisema Mfinanga. Alidai kwamba mpaka sasa zaidi ya watu 70 wamepoteza maisha kutokana na kuibuka kwa migogoro kati ya wawekezaji na wananchi wa maeneo ya machimbo ya madini.
Mfinanga ambaye alikuwa na zaidi ya wenzake 20 kwenye mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika Kawe, alisema wametoa msimamo huo kutokana na tukio la hivi karibuni la polisi kuwapiga risasi na kuwaua watu watano kwenye Mgodi wa North Mara, wiki iliyopita.
Aliitaka serikali ifanye uchunguzi huru na wa kina ili kujua chanzo na kuweka mkakati madhubuti utakaozuia mauaji hayo yasitokee tene.“Tusiishie kuwakamata watu wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo. Ila kitu kinachotakiwa ni kufanya uchunguzi wa kina ili kujua nini chanzo cha mauaji hayo,” alisema Mfinanga.
(Chanzo- Mwananchi)
Thursday, May 26, 2011
UVCCM Arusha watoa tamko kali: Wataka Lowassa, Rostam na Chenge (Mapacha watatu) wang'olewe.
TAMKO LA VIJANA WA CCM MKOA WA ARUSHA TAR 25/05/2010
Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi na Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha.
Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:-
Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba. Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa watanzania. Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa kifisadi ambao ni Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania. Pia tunasisitiza kuwa Andrew
Chenge aondolewe kwenye kamati ya maadili ya CCM mara moja na wakati huohuo Edward afukuzwe kwenye kwenye ya uwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya umoja wa vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunamtaka kuwa James Millya ambaye ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoa wa Arusha ajiuzulu mara moja na tunatamka rasmi kumfukuza kwenye UVCCM mkoa wa Arusha ili apate fursa ya kwenda kuwa tumikia mafisadi.
Tunamtaka James Millya aache kufikiria kwa kutumia tumbo na badala yake atumie kichwa.
Pia tumeshaandika barua yenye kumbukumbu namba kumb. Ars/Malalamiko/01 kwenye Chama kuelezea namna alivyo mnafiki, mfitini,mwongo na namna asivyo jali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha.
Vilevile tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa Ally Bananga anaetumiwa na Millya pamoja na mafisadi hana nafasi yoyote ndani ya Umoja wa vijana wa CCM kuanzia kwenye tawi hadi Taifa.
Kwamantiki hiyo Ally Bananga aache mara moja kuganga njaa kwa kutumia jina la UVCCM. Pia tunampa onyo kali Catherine Magige aache mara moja kutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hatujatumia haki yetu ya kikanuni ya kumsimamisha Ubunge. Tunajua kuwa amepata ubunge kwa nguvu za kifisadi kupitia UVCCM.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunakiomba chama cha cha mapinduzi kiwafukuze mara moja makatibu wa UVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwa kushiriki mandalizi ya maandamo haramu na kwa kukataa wito wa chama wa kwenda kutoa ushahidi wa malamiko yao kuhusu mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa. Kitendo hicho cha kukataa wito wa Chama ni dharau na ukosefu wa maadili.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunatamka kwamba ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha tunamtaka Onesmo Nangole ajiuzulu mara moja kwa kuwa anafanya kazi ya Fisadi Edward Lowasa na si ya CCM. Kitendo chake yeye cha kufanya kazi ya mafisadi na si ya CCM kimetupelekea kupoteza majimbo mawili kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunatamka kwamba Mhe. Mary Chatanda (MB) ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Arusha ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa wa Arusha. Amefanya mengi ya maana na wa-CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi ya chama chetu wanatambua hilo.
Pia tunawaomba CCM Taifa waendelee kumwacha hapa Arusha ili aendelee kukijenga chama na kukomesha mafisadi pamoja na dagaa wao.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunatamka rasmi kumtambua Ndugu. Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wa baraza kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha mkoa wa Arusha.
Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamo wetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa Tanzania.
Tunashauri CCM Taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chamatawala katika nchi hii.
TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWETU MWIKO
KAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAA
KITADUMU CHAMA CHA MAPINDUZI BILA MAFISADI
NYAMONGO ni huzuni yetu, aibu yetu.
Ndugu zangu,
PICHA ya jeneza lililotelekezwa barabarani imeongea zaidi ya maneno milioni moja. Kwa Watanzania, imetutia simanzi, imetutoa machozi. Ndani ya jeneza hilo pichani kuna mwili wa marehemu Emmanuel Magige iliyotelekezwa kijijini Nyakunguru, Tarime. Emmanuel Magige hakuwa jambazi. Ni Mtanzania mwenzetu mwanakijiji wa kawaida. Aliyetelekezwa si Magige tu, kuna maiti nyingine tatu.
Mauaji ya Nyamonngo yanatukumbusha Arusha, yanatukumbusha Mbarali. Yanatutia hofu mpya pia. Hatujui kesho yatafanyika wapi.Kupunguza aibu hii ni kwa wote waliohusika na mauaji haya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Jeneza la Emmanuel Magige lililotelekezwa barabarani ni kielelezo cha mahali tulipofikia. Kuna chuki inajengeka. Na katika tofauti zetu hizi za kiitikadi tusifike mahali tukashindwa kuongea kama Watanzania. Tusifike mahali tukachochea machafuko makubwa ya kijamii. Wanasiasa wana jukumu la kutanguliza busara katika kila maamuzi wayafanyao.
Na tuyalaani vikali mauaji ya Nyamongo. Tusipoyalaani nasi tutalaaniwa. Na Mungu huyu anatupenda Watanzania, kuna tunachoonyeshwa. Na tuzisome kwa makini alama hizi za nyakati. Na Miungu yetu, mizimu ya mababu zetu, inatupenda pia. Walikolala mababu zetu, nao wanaturajia tulaani kitendo hiki, maana, hata katika mila na desturi zetu, Waafrika hatutelekezi maiti zetu. Tunazizika.
Ndio, kwa jadi yetu, Waafrika tunahesabu wafu wetu, tunawatambua kwa majina, tunawaombea kwa imani zetu. Ndio, tunawazika wafu wetu. Kwa heshima zote.
Kwa desturi, Watanzania hatupendi kuwa katika hali ya kudharauliwa na kutothaminiwa kwa utu wetu tukiwa hai. Na kamwe, tusikubali Watanzania wenzetu wasithaminiwe wakiwa katika hali ya umauti. Na hilo ni Neno la Leo.
Temba DB
© MMXI
CHUO Kikuu Tumaini Iringa.
Hapa ni darasani sio bungeni.
Computer Lab
Mandhari nzuri
New Library and Computer Lab
Mandhari tulivu kwa masomo
Computer Lab
Jengo la msalaba lililopachikwa jina la Multipurpose kutokana na shughuli zake nyingi.
KARIBU SANA CHUO KIKUU TUMAINI., ILA ADA KUBWA.
Wednesday, May 25, 2011
MAFISADI CCM watorosha sukari.
SUKARI ya kifisadi zaidi ya tani 50 iliyofichuliwa na kada wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoani Iringa Thomas Nyimbo (Pichani) mbele ya mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe mjini Makambako wilaya ya Njombe wakati wa mikutano ya Chadema mikoa ya nyanda za juu kusini imeyeyuka.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya siku Nyimbo alisema kuwa sukari hiyo ambayo ilifichwa mjini Makambako na mmoja kati ya vigogo wa CCM kwa ajili ya kuiuza kwa magendo waliitorosha siku ya pili baada ya mkutano mkubwa wa Chadema mjini Makambako .
Alisema kuwa sukari hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika maghara ya kuhifadhia mbolea ya serikali mjini Makambako na kumtaja mmiliki wa maghala hayo (jina limehifadhiwa ) kuwa ndiye anayejihusisha na mtandao wa kifisadi kupitia kigogo huyo wa CCM ngazi za juu.
Hata hivyo Nyimbo alisema kuwa kazi ya kuhamisha sukari hiyo imefanywa kwa siri kubwa na kuwa suala hilo kwa viongozi wa mji wa Makambako pamoja na jeshi la polisi makambako linafahamu vizuri suala hilo la sukari hiyo na mmiliki wake .
Nyimbo alisema kuwa sukari hiyo iliondolewa kwa siri chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi Makambako japo hadi sasa suala hilo limeendelea kubaki siri na hakuna hatua zozote zilizochukulwa. (Imeandikwa na Francis Godwin kutoka Iringa)
MKANGANYIKO wa leo:...HIVI hatuwezi kutafuna biskuti huku tunatembea?!!
Gari ya serikali ikiwa na namba zaidi ya moja, moja ikiwa ni STK na ya pili ikiwa ni ya Naibu Waziri Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo (NW HVUM)
TUTAFAKARI PAMOJA....!!!! TUCHUKUE HATUA PAMOJA....!!!!
Tuesday, May 24, 2011
RAIS na bembea, watanzania na umaskini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kulia) akiwa katika bembea pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete (wa pili kushoto) katika moja ya ziara zake za nje. Pembeni ni wenyeji wao.
HIVI inawezekana kweli mtu ambaye tunatarajia awe mwakilishi wetu anakuwa na mambo ya kipumbavu hivi? Sijui watanzania tunaburuziwa wapi.
TUTAFAKARI PAMOJA, TUCHUKUE HATUA PAMOJA.
HIVI inawezekana kweli mtu ambaye tunatarajia awe mwakilishi wetu anakuwa na mambo ya kipumbavu hivi? Sijui watanzania tunaburuziwa wapi.
TUTAFAKARI PAMOJA, TUCHUKUE HATUA PAMOJA.
MKANGANYIKO wa leo. watu, ardhi na siasa safi, ni nini tumekosa watanzania?
TUNAADHIMISHA miaka hamsini ya uhuru tukiwa kama taifa lililotelekezwa katikati ya msitu wa matunda. Tunajua tu kulalamika na kuto kutambua wajibu zetu. Hatuelewi kwamba Tanzania ni yetu sote na si ya akina Kikwete au CCm yake.
Siasa safi ni uadilifu, je viongozi wetu ni waadilifu?
TUTAFAKARI PAMOJA!!!!! TUCHUKUE HATUA PAMOJA!!!
Siasa safi ni uadilifu, je viongozi wetu ni waadilifu?
TUTAFAKARI PAMOJA!!!!! TUCHUKUE HATUA PAMOJA!!!
Monday, May 16, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)