Uteuzi TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwataarifu kuwa Ofisa Habari wake, Boniface
Wambura ameteuliwa na SZhirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa
watakaoshughulikia masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake
zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo
za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika Novemba 11,
2012.
Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia habari kwenye fainali hizo. Wengine
ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF, Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.
Wambura atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye Kamati ya Maandalizi ya fainali hizo, kitu ambacho TFF
inajivunia kutoa mwakilishi kwenye moja ya mashindanoi makubwa ya mpira wa miguu Tanzania.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga ameelezea uteuzi huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri ambayo Wambura
amekuwa akiifanya tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka 2011.
“Taarifa zake mbalimbali zimeifanya Tanzania iwe inang’ara CAF na hata FIFA kwa kuwa kwa sasa
wanajua kila kinachoendelea kwenye soka la Tanzania,” alisema Rais Tenga na kumtakia Wambura kila la
kheri kwenye kazi hiyo atakayoifanya kwa takriban siku 14.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, akizungumza kwa niaba ya Sekretarieti, amemtakia Wambura kazi
njema na kwamba awe kioo cha mabadiliko makubwa yanayoendelea kwenye soka la Tanzania.
Wambura alijiunga na TFF Januari, 2011 akiwa mmoja wa waajiriwa watatu wapya kwenye Shirikisho
baada ya wsatendajiu wengine wawili kumaliza muda wao wa mikataba.
Wambura ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye ameshafanya kazi kwenye vyombo mbalimbali
kuanzia kazi ya uandishi hadi Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo ambalo alikuwa akifanya kazi
kabla ya kujiunga na TFF
Mahmoud Garga (CAF)
Boniface Wambura (Tanzania)
Arlindo Macedo (Angola
Mama Kikwete Mgeni Rasmi
The
Month of Women Entrepreneurs Committee in collaboration with the
International Labor Organization’s Women Entrepreneurship Development
and Economic Empowerment Project (YEF-WEDEE) and WAMA Foundation is once
again organizing the Month of Women Entrepreneurs (MOWE 2012) to
promote the Decent Work Agenda, women entrepreneurs and entrepreneurship
as a source of employment to men and women including the young people
of Tanzania
Azam Yafukuzia Kuongoza Ligi
Release No. 174
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Oktoba 23, 2012 AZAM YAFUKUZIA USUKANI WA LIGI
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Oktoba 24 mwaka huu) kwa mechi nne za raundi ya tisa huku Azam ikiusaka usukani wa ligi hiyo ikiwa mwenyeji wa Ruvu Shooting. Mechi hiyo namba 60 ambayo kama Azam itashinda itafikisha pointi 20, hivyo kuwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000. Yanga itawakaribisha Polisi Morogoro ambao ndiyo wa mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom hivi sasa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Alex Mahagi kutoka Mwanza ndiye atakayepuliza filimbi kwenye mechi hiyo namba 62. Waamuzi wasaidizi ni Frank Komba na Michael Mkongwa, wote kutoka Iringa wakati mwamuzi msaidizi ni Oden Mbaga anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wa Dar es Salaam. Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya African Lyon ya Dar es Salaam ambao ni wageni wa Coastal Union inayonolewa na Hemed Moroco. Nayo Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko kwenye mashamba ya miwa Turiani mkoani Morogoro. MTIBWA SUGAR, JKT RUVU SASA KUCHEZA NOV 7 Mechi namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu iliyopangwa kuchezwa Novemba 3 mwaka huu Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, sasa itafanyika Novemba 7 mwaka huu. Mabadiliko hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza mechi namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe Oktoba 3 mwaka huu lakini ikabadilishwa ili kutoa fursa kwa mechi za Super Week zilizooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport cha Afrika Kusini. VITAMBULISHO FAINALI ZA AFCON 2013 MWISHO NOV 7 Waandishi wa Habari wanaotaka kuripoti fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini wanatakiwa kutuma maombi ya kupatiwa vitambulisho (Accreditation) kabla ya Novemba 7 mwaka huu. Maombi hayo yatumwe Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupitia CAF Medial Channel inayopatikana katika mtandao wa Shirikisho hilo wa www.cafonline.com FDL KUANZA KUTIMUA VUMBI OKT 24 Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 24 mwaka huu) kwenye viwanja mbalimbali nchini. Kundi A kutakuwa na mechi tatu ambapo Burkina Faso itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati JKT Mlale itakuwa mwenyeji wa Small Kids kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea. Nayo Kurugenzi itaumana na Majimaji katika Uwanja wa Wambi ulioko Mufindi mkoani Iringa. Kundi hilo litamaliza raundi ya kwanza keshokutwa (Oktoba 25 mwaka huu) kwa mchezo kati ya Mkamba Rangers na Polisi Iringa utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Mechi za kundi B kwa kesho ni Ndanda dhidi ya Transit Camp katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Villa Squad itakipiga na Moro United kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors v Tessema (Mabatini, Mlandizi) na Polisi Dar v Ashanti United (Uwanja wa Chamazi). Kundi C kesho (Oktoba 24 mwaka huu) ni Kanembwa FC v Polisi Dodoma (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Mwadui v Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

TBL Yajenga Visima Handeni
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni,akipokea mfano wa hundi ya sh 40.5 milioni kutoka
kwa Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), Steve Kilindo kwa ajili yakuendeshea mradi wa uchimbaji wa
visima 15 vya maji katika vijiji vitano vya Kata ya Kwangwe,Wilaya ya
Handeni,Mkoa wa Tanga, mradi huo unaotazamiwa kukamilika mara baada ya
miezi mitatu.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Steve Kilindo (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Kata ya Kwamgwe, wilayani
Handeni, Tanga, Shariffa Abebe mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil.
40.5 akipokea hundiya sh 40.5 zilizotolewa na kampuni ya TBL kwa ajili
ya kuchimba visima 15 katika vijiji vitatu vya kata ya Kwamgwe.
Diwani wa kata ya Kwamgwe Wilaya ya Handeni,Shariffa Abebe akiishukuru
Kampuni ya TBL kwa kutoa kiasi cha sh 40.5 milioni kwa ajili ya
kuchimba visima 15 vya maji katika vijiji vitatu vya Kata ya Kwamgwe.
Diwani wa Kata ya Kwamgwe,Wilaya ya Handeni,Mkoa wa Tanga,Shariffa Abebe
akipitia ratiba ya hafla ya uzinduzi wa mradi wa uchimbaji wa visima 15
katika vijiji vitatu vya kata hiyo vilivyofadhiliwa na kampuni ya TBL
iliyotoa kiasi cha sh 40.5 milioni. Mradi huo ulizinduliwa na Mkuu wa
Wilaya ya Handeni,Muhingo Rwenyemamu aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Chiku Gallawa.
Endless Crop Levy Worries Iringa Farmers
THE ever-demanded crop levy is still a
burden to farmers in Iringa, who claim to be compelled to endure with
double charges by authorities. Speaking before the Constitution Review
Team mid this week, a farmer at Mtwivila Ward said the payments were too
much for the farmers to afford.
"We always pay the levy to the
authorities where our farms are located," she said. She was upset that
the same levy was slapped on the produce that she ferried home from the
farm. She wanted the new constitution to restrict crop levy on poor
farmers.
"It is not fair to subject a farmer to
payment of between 70,000 and 80,000/- as crop levy, yet I am not a
trader, the food is for home consumption," she lamented.
The farmer further lamented for another
Housing tax, which was executed by the local authorities in the
district.
"As a widow I worked hard to improve my income and used some of it to
renovate my house, which caused me trouble," she said. She claimed that
the land authorities have increased the House tax from 6,000/- to
15,000/- after she renovated her house.
Soma zaidi...
www.kwanzajamii.com/?p=4073
Write Own Constitution, Warioba Tells Wananchi
THE Chairman of the Constitution Review
Commission and former Prime Minister, Judge Joseph Warioba began his two
days working visit in Iringa on Thursday.
Speaking to the residents of Kitwiru and
Ruaha wards in Iringa Municipality, he urged them to make sure that
they are the ones who write the new constitution. He is in Iringa to
participate in the exercise by observing and helping in the processes of
collecting views in the region.
"We make interventions to get
clarifications from the speakers so that these ideas are clear to all of
us who are going to sort them out," he said.
The chairman had a number of times asked
some speakers to clarify on certain opinions that they presented to the
Constitution Review Commission Team that he joined here, which is
continuing to collect views in Iringa Municipality.
Soma zaidi...
www.kwanzajamii.com/?p=4077
UN Tanzania Yahamasisha Upandaji Miti
Afisa Habari wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Bw. Austin Makani akizungumza
na wakazi wa kata ya Pugu akizungumzia kwanini Umoja wa Mataifa katika
wiki hii ya maadhimisho ya miaka 67 tangu kuanzishwa pamoja na mambo
mengine imeamua kutilia mkazo suala la Utunzaji wa Mazingira kwa kuwa ni
moja ya maeneo muhimu unapozungumzia suala zima la kutoa elimu juu ya
mabadiliko ya Tabia
nchi
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro (wa pili kulia) aliyemwakilisha mgeni rasni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Stella Karegesya UNV Program Officer Tanzania (kulia) Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Fresh Bw. Ally Maguno, Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw. Justin Nyangwe na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinyamwezi Bw. Mohamedi Abdalah aliyemwakilisha Diwani wa Kata ya Pugu katika meza kuu
Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw. Justin Nyangwe akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi ambapo ametoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuwapa umuhimu wakazi wa Pugu kwa kuchukua hatua ya kushirikiana nao katika suala zima la kuboresha mazingira na wanaahidi kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira

Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa
UNDP Dkt. Amani Ngusaro (wa pili kulia) aliyemwakilisha mgeni rasni
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akitoa nasaha zake katika wiki
ya maamdhisho ya Umoja wa Mataifa ambapo Umoja huo ulikwenda kufanya
kampeni ya kuhimiza wananchi kutunza mazingira katika Kata ya
Pugu
Monday, October 22, 2012
JK Katika Mkutano Wa UWT Taifa
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa
Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akisalimiana na wakongwe wa UWT katika ukumbi wa Chuo cha
Mipango mjini Dodoma baada ya kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT)
PICHA NA IKULU
Mkurugenzi Mpya Wanyamapori
Prof. Alexander Nyangero Songorwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Prof.Jafari Ramadhani Kideghesho, Mkurugenzi Msaidizi, Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
TAARIFA KWA UMMA
VIONGOZI WAPYA WA IDARA YA IDARA YA WANYAMAPORI
WATEULIWA
Profesa Alexander Nyangero Songorwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori (Wildlife Division ) kuziba nafasi iliyokuwa wazi.
Kabla ya kuteuliwa Profesa Nyangoro alikuwa Profesa Mshiriki katika
Usimamizi wa Wanyamapori, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),
Morogoro. Pia ndiye aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo ya Usimamizi wa
Wanyamapori SUA.
Wakati huohuo, Profesa Jafari Ramadhani Kideghesho ameteuliwa
kuwa Mkurugenzi Msaidizi, kuiongoza Sehemu ya Matumizi Endelevu ya
Wanyamapori (Sustainable Utilisation of Wildlife Section). Kabla ya uteuzi
huo Profesa Ramadhani alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa
Wanyamapori katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.
Uteuzi huo umetekelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Bibi Maimuna Tarishi kwa mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa kifungu cha 6
(1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002. Utekelezaji wa
uteuzi huo ni kuanzia tarehe 24 Septemba 2012.
Mkurugenzi mpya wa wanyamapori, Profesa. Songorwa, ni msomi katika fani
ya Wanyamapori. Anayo shahada ya kwanza (B.Sc.) ya Sayansi katika Zoolojia
na Ekolojia ya Wanyamapori ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (mwaka 1987),
Shahada ya uzamili (MSc) katika Mipango na Maendeleo Vijijini ya Chuo
Kikuu cha Guelph, Ontario, Canada (1994) na shahada ya uzamivu (PhD) katika
Uhifadhi Maliasili ya Chuo Kikuu cha Lincoln, New Zealand (1999).
Kabla ya kujiunga na SUA mwaka 2001, Prof. Songorwa alikuwa mwajiriwa
wa Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzia mwaka
1982.
Akiwa Wizarani Profesa Songorwa alihudumu katka nafasi mbali mbali
zikiwemo Askari Wanyamapori, Mkuu wa Kanda na Msaidizi wa Mkuu wa
Mradi katika Pori la Akiba la Selous. Pia alihudumu kama Afisa Mwandamizi
katika Mradi wa Uhifadhi Shirikishi wa Wanyamapori, Makao Makuu, Dar es
salaam.
Naye Profesa Kideghesho siyo mgeni katika Idara ya Wanyamapori. Kabla ya
kujiunga na na SUA mwaka 1999 Prof. Kideghesho alikuwa mwalimu katika
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (CAWM-Mweka), Moshi
kuanzia 1993.
Kitaaluma Prof. Kideghesho ana shahada ya kwaza (B.Sc.) katika Kilimo ya
SUA (1993), Shahada ya Uzamili (MSc) katika Biolojia ya Uhifadhi ya Chuo
Kikuu cha Kent, Uingereza (1996), na Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Norway kilichopo mjini Trondheim
(2006).
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Simu 0784 468047
22 Oktoba 2012

Lowasa Mgeni Rasmi VICOBA
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA
Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA
Tanzania.Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro
Mahanga na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA
Tanzania,Aldo Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi
wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na
Wajasiliamali wa VICOBA uliyofanyika kwenye
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia ni Mgeni
Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh.
Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh
Assaa Simba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.
Burudani ya Ngoma za Asili.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA
Tanzania,Bi. Magreth Mapunda akisoma Risala ya Chama chao hicho mbele
ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa
Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda (kushoto) akikabidhi Risala hiyo kwa Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba akisalimia Wanachama wa VICOBA Tanzania.
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akizungumza machache
kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza na Wanachama wa VICOBA.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya wanachama wa VICOBA Tanzania wakati hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Katika Hobuba yake,Mh. Lowassa aliwapongeza wana VICOBA
kwa kuweza kujiajiri,kwani tatizo la ajira nchini bado ni tatizo kubwa
na ni bomu linaweza kulipuka wakati wowote.Maonyesho hayo yataendelea
mpaka jumamosi ijayo Oktoba 27.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto)
akiteta jambo na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akicheza muziki sambamba na Wanachama wa VICOBA Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Biashara ya Miaka Kumi yam Wajasilia Mali wa VICOBA tangu kuanzishwa kwakwe,iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akibonyeza kitufe kwenye kompyuta ikiwa ni ishara ya Uzinduzi rasmi wa
Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono Wanachama wa VICOBA
wakati wa kuwaaga mara baada ya kufanya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka
Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na baadhi ya Wanachama wa VICOBA mara baada ya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasilia mali wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana
na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Wanachama wa VICOBA wakijiburudisha kwa kucheza Muziki.
Maandamano ya Wanachama na Wajasiliamali wa VICOBA yakipita Mbele ya Mgeni Rasmi,ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
No comments:
Post a Comment