Thursday, January 05, 2012

HAMAD afukuzwa rasmi CUF

Mhe Hamad Rashid,Mbunge wa Jimbo la Wawi akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Ukumbi wa Mkutano muda mfupi baada ya kufukuzwa Uanachama wa CUF,na Mkutano wa Baraza Kuu la CUF, unaofanyika katika Hoteli ya Mazsons Shangani Unguja jana.  

Waandishi wa habari wakiwa katika viwanja vya Hoteli ya Mazsons Shangali wakisubiri kupata taarifa ya yaliojiri ndani ya Kikao cha Baraza Kuu

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF, Shoka Khamis Juma, ambaye ni mmoja wa Mwanachama aliyefukuzwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la CUF, akizungumza na waandishi  baada ya kutoka katika kikao kumaliza kujieleza. Picha Zote na Othman Mapara
 
BARAZA Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) limemvua uanachama Mbunge wa Wawi na Mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho, Hamad Rashid Mohamed, kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama na hivyo kupoteza sifa za uanachama.

Akitangaza uamuzi huo katika Hoteli ya Manson Mji Mkongwe jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro alisema mbali na Hamad Rashid, pia baraza hilo limewavua uanachama wajumbe wengine watatu wa Baraza Kuu.

Wajumbe hao ni Doyo Hassan Doyo kutoka katika Mkoa wa Tanga, Juma Sanani ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi na Shoka Khamis Juma, aliyewahi kuwa Mbunge wa Micheweni kwa tiketi ya CUF.

“Baraza Kuu la CUF limewafukuza viongozi hao baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili kutoka wajumbe wa Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka wajumbe Zanzibar,” alisema
Mtatiro.

Mjumbe mwingine: Yasin Mrotwa amepewa onyo kali na karipio huku na kwa mujibu wa Mtatiro, anaendelea kuchunguzwa na Baraza Kuu.
Seif dikteta! Baada ya kuvuliwa uanachama, Hamad Rashid alizungumza na waandishi wa habari na kumuita Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, dikteta na kiongozi asiyeheshimu uamuzi wa Mahakama.

“Sisi tumeweka pingamizi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa mkutano wa Baraza Kuu na hati ya Mahakama ipo wanayo...sasa nawashangaa wanakiuka sijui kwa nini?” Alihoji Hamad Rashid.

Alisema watakwenda tena mahakamani Februari 14 kusikiliza shauri lao la pingamizi la kikao hicho.

No comments:

Post a Comment