Wednesday, January 04, 2012

BARABARA ya Kilwa kujengwa upya



Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli akiongea kwa msisitizo wakati alipoongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Wizara hiyo kuhusu upanuzi wa barabara ya Kilwa Road yeny kilomita 5.1 kwa kiwanga cha lami itakayojengwa na mkandarasi Kajima Corporation. Barabara hiyo inarudiwa kujengwa kwa mara ya pili baada ya kampuni hiyo kubonronga katika ujenzi wa awali, Waziri Magufuli ameongeza kwamba Mkandarasi ataondoa tabaka la lami katika urefu wa Kilomita 5.1 na tabaka jipya la lami lenye unene wa sentimeta 7 akitumia lami yenye kiwango cha ugumu cha 40/50 na kokoto za ukubwa wa milimita 20. Yaani zege la lami (Asphalt Concrete) lenye kokoto za ukubwa wa milimita 20 (AC20), lami iliyoimarishwa zaidi itafikiriwa kutumika sehemu za barabara zenye kubeba mzigo mkubwa zaidi, katika picha kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mh. Masaki Okada.

No comments:

Post a Comment