Tuesday, January 31, 2012

Siku Nyerere Alipocheka Sana Ikulu!


Inasimuliwa, kuwa katika siku za mwanzo za kukaa kwake Ikulu Nyerere alijulishwa kuwa angekuja Balozi mpya wa Swaziland kujitambulisha. 
Ikafika siku, mara Julius Nyerere akamuona Mheshimiwa Balozi anaingia akiwa ametinga na vazi la jadi la Waswazi. Mkononi kashika bakora pia. Kwa macho ya Nyerere alimwona Mheshimiwa kama mtu aliyeingia Ikulu nusu uchi. Nyerere akabanwa na kicheko. Alikivumilia. 

Mgeni alipoondoka , Nyerere akawageukia wasaidizi wake na kuangua kicheko. Alisema;
"Jamani, mbona hamkuniambia mapema kuwa Balozi angeingia Ikulu kwa staili ile?" Nyerere akaendelea kucheka, na wasaidizi wake pia. Wote wakacheka sana.  Mheshimiwa Balozi wa Swaziland hajapata kujulishwa juu ya kicheko alichokiacha nyuma, pale Ikulu ya Magogoni.

KIPANYA



" Oh, Mama Kabwela UNO!"

Reactions::

Rais Wade wa Senegal kuwania urais tena

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal
Rais Abdoulaye Wade wa Senegal
 
Mahakama Kuu ya Senegal imetupilia mbali kesi ya rufaa ya vyama vya upinzani na kuthibitisha kuwa Rais Abdoulaye Wade anaweza kugombea kiti cha urais wa nchi hiyo kwa mara ya tatu.
Upinzani umesema katiba ya nchi hiyo imeweka kikomo cha mihula miwili, lakini mahakama hiyo imesema Bwana Wade hafungwi na sheria hiyo kwa sababu, sheria hiyo ilipitishwa akiwa katika muhula wake wa kwanza.

Vodacom Foundation yakabidhi madarasa 3 na madawati 100 S/Msingi Ruvu Darajani


Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba kushoto akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo mkoani pwani,mara baada ya kuwakabidhi rasmi vyumba vitatu vya madarasa na madawati 100 kwa ajili ya shule hiyo,Msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 98.
Haya ndiyo madarasa ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani yaliyojengwa na Vodacom Foundation.
Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu shule za Msingi,Zuberi Samataba mwenye suti akiongea jambo na 0fisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,walipowasili katika shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madarasa matatu na madawati 100 uliotolewa na Vodacom Foundation katika shule hiyo na kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 98.
Hili ndilo jiko la wanafunzi wa shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani,Taswira hii imepigwa na mpiga picha wetu katika makabidhiano ya vyumba vitatu vya madarasa pamoja na madawati 100 vilivyokabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki na Vodacom Foundation kwa ajili ya shule hiyo,wadau jitokezeni msaidie hata kujenga jiko hilo.
 
Kikundi cha ngoma cha wazazi wa mkoa wa Pwani wakitumbuiza wakati wa makabidhiano rasmi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na madawati 100 vilivyokabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki na Vodacom Foundation kwa ajili ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani,Msaada huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 98,
 
0fisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na madawati 100 vilivyokabidhiwa rasmi na Vodacom Foundation kwa ajili ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani,Msaada huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 98,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa shule za msingi Wilaya ya Bagamoyo na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mary Nzowa.

Chadema wazindua kampeni Uzini, Zanzibar


 
Mkutano wa uzinduzi kampeni  za CHADEMA Uzini leo

Mbowe, Dk.Slaa na viongozi Chadema wahudhuria mazishi kabla ya mkutano uzini Zanzibar











 
Viongozi wa CHADEMA wamehudhuria maziko kwanye wadi ya Bambi eneo jirani na ulipofanyika mkutano wa uzinduzi kampeni.

NIPO kwenye mitihani iliyoanza mapema jana Tar 30 Jan. Niombeeni

Monday, January 23, 2012

Chadema na serikali waendelea na maongezi juu ya katiba, Dk.Slaa ahudhuria

  
Rais Kikwete akimkaribisha Dk.Slaa na viongozi wa CHADEMA ikulu jana usiku kwa mazungumzo tena kuhusu suala la katiba
 
  
Wanapitia makabrasha kifungu kwa kifungu
 

Dk.Slaa akitoa ufafanuzi juu ya masuala ambayo chama chake kinaamini ni muhimu kuzingatiwa kwa maslahi ya wananchi
 
 
Maongezi yanaendelea, kifungu kwa kifungu.saa tatu walikaa katika vikundi kile cha CHADEMA na kile cha serikali kujadili misimamo na makubaliano, kisha kikao kiliendelea hadi saa 5:30 usiku.tunasubiri taarifa rasmi
Picha kutoka IKULU

Taswira Kutoka ikulu Za Kumalizika Kwa Kikao Maalum Cha Rais Jakaya Kikwete na Viongozi wa CHADEMA Usiku Ikulu

 Rais Jakaya Kikwete akiagana na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa(Kushoto) Usiku wa Kuamkia leo baada ya Kumalizika kwa Kikao Maalum Cha Viongozi wa Chadema na Rais Jakaya Kikwete kilichokua kikijadili Mchakato Wa Katiba Mpya

Rais Jakaya Kikwete akiondoka Muda Mfupi baada ya Kumalizika Kwa Kikao Chake Usiku wa Kuamkia Leo na Viongozi Waandamizi wa CHADEMA Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mh Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa Pamoja na Wajumbe Wengine Waandamizi

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mmoja wa Wajumbe Waadamizi wa CHADEMA Profesa Mwesiga Baregu Muda Mfupi baada ya Kumalizika kwa Kikao Cha Rais Jakaya Kikwete na Viongozi Waandamizi wa CHADEMA ikulu Jijini Dar es Salaam Usiku wa Kuamkia Leo.Picha na IKULU

Sunday, January 08, 2012

URAIS 2015 Chadema Kwafukuta


Katibu Mkuu wa chadema, Dk Willibroad Slaa

















Dk Slaa, Mbowe, Zitto hapatoshi
 

FUKUTO la Urais mwaka 2015 ndani ya vyama vya siasa linazidi kupamba moto, huku majina ya makada wanaowania nafasi hiyo kupitia chama kikuu cha upinzani nchini Chadema, yakianza kuanikwa.

Ikiwa imebaki takribani miaka mitatu kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2015, makada mbalimbali ndani ya vyama, wameanza kupigana vikumbo kila mmoja kujaribu kujipanga ili achaguliwe kupeperusha bendera ya chama chake kwenye uchaguzi huo.

Ndani ya chama tawala CCM, taarifa zinadai kuwa baadhi ya wanasiasa wameanza kuunda mitandao huku wengine wakilaumiwa kuanza ‘kucheza rafu’ kwa kumwaga mamilioni ya fedha kwa lengo la kutekeleza mkakati huo.Tayari hatua hiyo imelaumiwa na baadhi ya makada ndani ya chama hicho kikongwe nchini huku wengine wakionya kuwa mbio za Urais mwaka 2015, zinatishia kuisambaratisha CCM.

Wakati heka heka hizo zikiendelea ndani ya CCM, habari kutoka ndani ya Chadema, zimetaja baadhi ya majina ya makada wa chama hicho, wanaopewa nafasi kubwa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Chadema, zimewataja watu hao kuwa ni  Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chadema ambaye pia aligombea urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi uliopita, Dk Willibroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Ingawa Zitto tayari ameweka wazi kuwa hatagombea kutokana na umri wake kuwa chini ya ule unaotambuliwa kikatiba kwa nafasi hiyo, bado ana matumaini kwamba kipengele hicho kinaweza kubadilishwa ndani ya katiba mpya.

Kwa mujibu wa katiba ya sasa, mtu anayewania Urais wa Jamhuri ya Muungano lazima awe na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea. Mwaka 2015 Zitto atakuwa hajafikisha umri huo na ‘atanusurika’ endapo tu katiba mpya itapunguza umri huo.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa picha halisi ya atakayewania nafasi ya urais kupitia chama hicho itadhihirika baada ya kukamilika kwa chaguzi za ngazi zote ndani ya chama hicho baadaye mwaka huu.

Mazingira mengine ambayo yanaweza kuathiri ama kuamua juu ya mgombea urais wa chama hichona kujiunga kwa wanachama wapya husasan kama baadhi ya vigogo watajiengua CCM na kuamua kujiunga na chama hicho.


Hofu ya makada wa CCM kutimkia Chadema inatokana na kundi kubwa la wanasiasa ndani ya chama hicho kutaka nafasi hiyo, hali itakayowafanya wengine kwenda vyama vingine kujaribu bahati zao.

Kutokana na idadi kubwa ya wanaCCM wanaotaka nafasi hiyo, baadhi ya watu wanadaiwa kuunda mitandao yenye malengo ya kuchafuana

CCM katika kikao chake cha Halmashuari Kuu (NEC) kilichoketi mjini Dodoma Novemba mwaka jana, kilikiri kuwa mvutano mkubwa wa makundi uliopo ndani ya chama hicho, chanzo chake ni Urais wa mwaka 2015.

Kwa upande wa Chadema, ingawa bado hakuna vita ya wazi wazi kama ilivyo ndani ya CCM, wanachama wake wameaanza kuzungumzia na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi huo.

Dk Slaa ambaye aligombea katika uchaguzi uliopita na kuibuka mshindi wa pili baada ya kupata asilimia 26 ya kura zote zilizopigwa, ndiye anayeonekana kupewa nafasi kubwa. Mwanasiasa huyo anaonekana kuwa bado anafaa kuwania tena nafasi hiyo kutokana na rekodi nzuri kwenye uchaguzi uliopita.

Katika uchaguzi huo, Dk Slaa alionesha kuyaelewa vyema matatizo ya Watanzania na kujaribu kueleza nini kifanyike kuondokana nayo, hali iliyowafanya wananchi wengi kuwa na imani naye.

Mbowe (50) ambaye aliwania kiti cha urais mwaka 2005 na kushika nafasi ya tatu, anatajwa kuwa anaweza kuwania tena nafasi kutokana na rekodi yake safi ya kukiimarisha chama hicho kunzia tangu kikiwa kichanga hadi kukiwezesha kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.


Wanachama wengine wa chama hicho wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamojan na John Shibuda ambaye mwaka juzi alichukua fomu za kuomba kuwania urais kupitia chama CCM, lakini baadaye alijitoa na kumuunga mkono mgombea wa chama hicho, Rais Kikwete.

Wengine ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Hata  hivyo Lema ambaye ametajwa kuwa mbunge bora kwenye moja ya mitandao ya kijamii nchini, aliliambia Mwananchi Jumapili juwa hana nia ya kuwania urais kupitia chama hicho mwaka 2015.

Alisema pamoja na kupata kura nyingi za watu waliomuunga mkono kwenye mtandao huo, alisema hatarajii kugombea nafasi hiyo ya urais ila akasisitiza kuwa ataweka nguvu zaidi kwenye ubunge."Nashukuru kwa kupata kura hizo, lakini sitarajii kuwania nafasi hiyo… Atakayeteuliwa na chama changu nitamuunga mkono," alisema.


Urais na migogoro
Imeelezwa kuwa migogoro mingi inayovikumba vyama vya siasa vikiwemo  NCCR -Mageuzi na CUF inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mbio za Urais mwaka 2015.

Tayari NCCR- Mageuzi na imetangaza kumvua uanachama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila na wanachama wengine 11 huku CUF kikimfukuza Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake, huku wanachama wengine wakipewa karipio kali.Hata hivyo, wabunge hao wamekataa kutambua kufukuzwa kwao huku wakifungua kesi Mahakama kuu kupinga  maamuzi vyama vyao.

Profesa Wangwe
Kuhusu nani anaweza kuteuliwa kugombea urais kupitia Chadema mwaka 2015, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuondoa Umasikini (Repoa), Profesa Samweli Wangwe alisema vyama vitakavyoteua wagombea ni lazima vichunguze kwa makini na kuona kwamba mgombea huyo  lazima awe na uwezo wa kuimarisha  uchumi ambao Watanzania wote wanaweza kushiriki katika kuujenga.

Alisema matatizo mengi ya kiuchumi yaliyopo nchini yanatokana na uchumi kusambaratika na wanaoshiriki katika kuujenga kuwa wachache."Mtu huyo lazima awe na mtazamo wa kiuchumi na ili mabadiliko hayo yawepo ni lazima ujengwe uchumi ambao watu wote pamoja na masikini wata-participate  (watashiriki).

Lakini akasema vyama vya upinzani hususan Chadema ambayo ilionekana kufanya vizuri katika uchaguzi uliopita, kitategemea kufanya vibaya kwa CCM ili kiweze kupata ushindi.
"Ili mgombea wa Chadema aweze kuchaguliwa itategemea sana kufanya vibaya kwa serikali ya CCM… Lakini ikifanya vizuri, itakuwa ni wakati mgumu kwao," alisema Profesa Wangwe.                                                     

Alipotakiwa kumtaja mtu ambaye anamuona kuwa anaweza kufanya vizuri kupitia Chadema, alisema ni vigumu kufanya hivyo kwa sababu hali hiyo inategemea sana ajenda ya chama hicho kwa mwaka 2015.

Alikiri kuwa Chadema kiliweza kuungwa mkono katika uchaguzi uliopita, lakini mipango yake kwa mwaka 2015 itategemea ajenda waliyo nayo na kufanya vibaya kwa serikali ya CCM.

Ndani ya CUF

Kwa upande wa CUF Mbunge wa Wawi aliyefukuzwa kutoka chama hicho hivi karibuni  Hamad Rashid amekataa kuuhusisha mgogoro huo na harakati zake za kutaka urais wa Zanzibar.

“Sikuyaanzisha mapambano haya kwa kutaka cheo. Mimi nilipewa uwaziri wakati wa Mwalimu Nyerere, lakini sikukubali, nikawaambia kuwa nitabaki tu na u-naibu Waziri wa Fedha” alisema Hamad na kuongeza;

“Mimi nimeshiriki kuanzisha CUF lakini sijawahi kuwa na uongozi mkubwa ndani ya chama, zaidi ya u-naibu Mkurugenzi tu. hata leo tukianzisha chama, wenzangu wakichagua viongozi, mimi niko radhi tu”.

Lakini kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar Ismail Jussa ametuhumu Hamad kufanya vurugu ndani ya CUF kwa lengo la kumpindua Maalim Seif katika nafasi ya ukatibu Mkuu, kisha kugombea urais.

 “Kama anapinga kutotaka cheo, basi Hamad anaanza kuchanganyikiwa. Mara ngapi katika matamshi yake amekuwa akitangaza kuitaka nafasi ya Ukatibu Mkuu. Anajidanganya,” alisema Jussa na kuongeza,

Friday, January 06, 2012

CUF: Why we threw out Hamad Rashid

Civil Union Front deputy secretary-general (Mainland) Julius Mtatiro briefs the media in Dar es Salaam yesterday on the party’s decision to expel Wawi MP Hamad Rashid Mohammed and three other members.






By The Citizen Reporters

Dar es Salaam. Wawi MP Hamad Rashid Mohammed has been kicked out of the Civil Union Front (CUF) for allegedly revealing party secrets and organising meetings without following party regulations.According to deputy secretary general (Mainland) Julius Mtatiro, the embattled MP published an official document in his recent book, Yaliyojiri.

But Mr Mohammed dismisses the claims, saying the offending letter was a personal communication between him and the party’s national secretary general, Mr Seif Shariff Hamad.

The party says it is preparing a letter informing Parliament of its decision to strip Mr Mohammed of his membership.   Other members sacked alongside Mr Mohammed are Mr Doyo Hassan Doyo, Mr Shoka Khamis Juma and Mr Juma Said Saani.The list of charges against the MP includes accusing Mr Hamad of failing to discharge his political duties because he is now part of the Government of National Unity in Zanzibar. “Joining the Government of National Unity was the party’s decision,” said Mr Mtatiro. “Accusing him means that he (Mr Mohammed) intends to divide the party.”

Mr Mohammed was also penalised for divulging party secrets. “He was not supposed to talk to the media...he was supposed to follow procedures to raise his concerns within the party,” Mr Mtatiro added. At a separate press conference, Mr Mohammed said he wrote the contentious letter to the CUF national chairman and wondered how he could be held to account for publishing his own letter, which he described as “very personal”.

 “That was my letter to him, so they can’t prosecute me for that,” said Mr Mohammed. “Did I publish official issues? If not, why should they punish me?”

According to the embattled MP, he expressed the same sentiments during the party’s general meeting but was blocked when he tried to follow through his accusations over embezzlement of party property.He also accused the party of disrespecting the judiciary by ignoring a court injunction barring the meeting which sacked him on Wednesday.

According to Mr Mtatiro, the group was found guilty of 11 offences after their cases were scrutinised by a number of party organs. Moreover, the sacking of the four members of the CUF National Council was in keeping with procedures set out in the party’s constitution.

Mr Mohammed contends that the sacking runs counter to the party’s constitution and the laws of the land, given that there was a court injunction against the meeting that sacked him and three others.

He vowed to fight for his CUF membership but would launch his own party should the courts uphold his expulsion.
Meanwhile, Mr Mohammed has received the backing of Deputy Leader of the Opposition in Parliament, Mr Zitto Kabwe (Kigoma North-Chadema).

He said sacking Mr Mohammed and the others was not the way to handle the problem, given that he had played a fundamental role in building the party. But CUF officials defended the decision, saying it was made in the interest of the party.
More criticism of the way CUF had handled the matter came from the leader of the CCM Youth wing (UVCCM), Mr Hussein Bashe. “This is not the proper way of disciplining somebody,” he said. “They (CUF) need to follow-up Mr Mohammed’s accusations instead of sacking him.”

The Registrar of Political Parties, Mr John Tendwa, suggested a review of election processes and the power of political parties to terminate membership. Political parties should make wise decisions in difficult circumstances, he said, or the country would be saddled with by-elections that cost billions of taxpayers’ money. A by-election in one constituency costs no less than Sh19 billion, he said, and a misunderstanding between one member and the party’s leadership should not be reason to “waste” public funds.

Mr Tendwa added: “We need to speak on this. My office is getting into trouble, the National Electoral Commission is also being disturbed and the government is using a lot of money unnecessarily. I think political parties need to be wise enough to avoid this.”

KIPANYA






UNAONAJE hii?

Thursday, January 05, 2012

DON'T Try This, at Home or at School, It is Not yet Recommended

VYAMA VIWAFIKIRIE WAPIGA KURA KABLA YA KUFUKUZA WABUNGE UANACHAMA

 

JOHN TENDWA


NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MSAJILI wa Vyama Vya Siasa, John Tendwa amesema kwamba ofisi yake inafikiria kuweza kubadilisha mifumo ya uchaguzi kwa kufikiria nafasi na haki za msingi za mpigakura dhidi ya chama kinapomfukuza uanachama mbunge.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Tendwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dares Salaam mara baada ya kuapishwa kwa viongozi wapya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ambapo alisema suala la kufukunzwa uanachama mbunge si geni lilishatokea hata katika mfumo wa chama kimoja.
Tendwa alitoa kauli hiyo mara baada ya kuulizwa swali la waandishi wa habari kuhusiana na kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid kufukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) hali ilimfanya kupoteza nyadhifa zake.
Ambapo Tendwa aliongeza kuwa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi inapotokea hali ya namna hiyo , alihoji kuwa mpigakura anafikiriwaje na chama juu ya sifa na haki za msingi dhidi ya chama.
“Tunafikiria tuweze kubadilisha mifumo hiyo ya uchaguzi kwa kuangalia mbunge na lazima tumfikirie mpigakura. Lazima tuangalie hali ya uchumi,” alisema Tendwa.
Alisema kitendo hicho kinasababisha gharama kwa serikali na wadau wengine mfano taasisi yake ambayo haikutarajiwa hata katika bajeti.
Tendwa aliongeza kuwa inapotakiwa kufanyika uchaguzi mwingine zinahitajika fedha nyingi ambapo wakati fulani alisema zinaweza kufikia sh. bilioni 19 ,hata hivyo hazitoshi.
Aidha alisema kuwa kifedha bado kitendo hicho kililiweka taifa katika mshtuko mkubwa kwa kuwa gharama ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine ni kubwa.
Alihoji kuwa maamuzi hayo yanapofanyika hawakuona fursa ya mpigakura ana haki gani ya kumtambua mbunge wake? je chama kinafaidika nini?
Alisema wataangalia kama taratibu zilifuatwa na chama ili waweze kushauri
Tendwa alisema suala hilo limekuwa ni tabia na desturi, hivyo ni jambo linapaswa kuangalia mbele ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa kwa kuwa kitendo hicho si kujenga demokrasia bali ni kuwafanya wanachama kuwa na utii wa uwoga ndani ya chama.
Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki ,John Cheyo akizungumzuia suala hilo alisema kitendo hicho cha kumwondoa mbunge katikati ya muda kinaleta matatizo makubwa ndani ya vyama , hivyo alivishauri vyama kuheshimu sheria na taratibu za mtu kumaliza muda wake.
Hivi karibuni Chama cha NCCR – MAGEUZI nacho kilimvua uanachama, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kwa madai ya utomvu wa nidhamu.

Salaam Za Mheshimiwa Zitto Kabwe(Chadema) Kwa Mbunge Wa CUF ismail Jussa Juu Ya Kuvuliwa Uanachama Mbunge Wa CUF Hamada Rashid

 

 Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Mheshimiwa Zitto Kabwe
--
Ndugu Jussa, Kama rafiki yako mkubwa na unajua ninavyomheshimu Maalim Seif Kama kiongozi thabiti.Leo nakwambia usilolipenda. Sio sahihi katika demokrasia Kama yetu kumfukuza Mbunge Hamad Rashid au hata wanachama wengine wa chama chenu cha CUF. 

Kama Maalim aliweza kumsamehe Salmin, aliweza kumsamehe Karume, aliweza kukubali kutangazwa kushindwa ilhali hata wewe unajua alishinda Urais wa Zanzibar iweje iwe muhali kumaliza tatizo hili dogo la Hamad Rashid? Hamad ana makosa lukuki. Nimefanya naye kazi Bungeni. Hamad pia ana mazuri mengi kafanya. Hamad amejitoa muhanga. Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kumfukuza uanachama ufikiriwe upya. That is my appeal to you as a friend and a fine politician
 
Zitto Kabwe(MB)

OUR kind of English

WHER you eat ANTIL you say....? My hope is that the signwriter was assigned to write "WHERE YOU EAT UNTIL YOU SAY..." Trust the signwriters!

KIPANYA Leo

BUKOBA KUJENGA KITUO CHA MABASI CHA KISASA

Mfano wa jengo la standi kuu ya mabasi itakayojengwa eneo la Kyakailabwa na manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na shirika la Mzinga linalomilikiwa na jeshi la wananchi wa Tanzania, jengo litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 25.8.

DARAJANI MADIBIRA

Daraja hili lenye urefu wa mita 500 limejengwa juu ya mto Lyandembera likiunganisha kitongoji cha Kinyasuguni na Mahango, Madibira, wilayani Mbarali mkoani Mbeya..Picha na Frank Leonard