Uamuzi wa pingamizi la kesi ya Ubunge ya Godbless Lema ni Jumatatu
Aliyekuwa
Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (katikati) akiwa na Mawakili,
Alute Mughway (kushoto) aliyesimamia kesi iliyomvua Ubunge na Mbunge wa
Singida Mashariki ambaye pia ni wakili katika kesi ya kupinga kuvuliwa
Ubunge wake, Tundu Lissu, katika msiba wao baba yao Alute na Lissu
aliyefariki hivi kaibuni jijini Dar es salaam na kisha kuzikwa nyumbani
kwao Singida. (picha ya Septemba 2012 via MjengwaBlog.com)
Uamuzi
wa pingamizi zilizowekwa na mawakili wa pande zote mbili katika kesi ya
uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA,
Godbless Lema utatolewa Jumatatu ijayo.Awali wa upande wa majibu rufani katika kesi iliyomng’oa madarakani Lema, Alute Mughwai ambaye ni Wakili wa wanachama watatu wa CCM, aliiomba Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali rufaa hiyo iliyowasilishwa kwao kwa kuwa ni batili na ina makosa mengi ya kisheria.
Habari za uhakika kutoka katika vyanzo vya habari ndani ya mahakama na kuthibitishwa na mmoja wa wanachama hao waliofungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kupinga Lema kuwa mshindi katika Jimbo la Arusha, Mussa Mkanga vilisema kuwa pingamizi hizo zitatolewa uamuzi siku hiyo.
Mkanga alipoulizwa kama ana taarifa ya kusomwa kwa pingamizi hizo, siku hiyo alikiri kupewa taarifa na mahakama na kueleza kuwa siku hiyo watakwenda kusikiliza uamuzi wa pingamizi zao.
“Mimi na wenzangu kama walalamikaji tumeshapewa taarifa na mahakama juu ya siku na tarehe ya kusomwa pingamizi hizo na tuko tayari kwa hilo,” alisema Mkanga.
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Hubert hakupatikana kuelezea taarifa hiyo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana, lakini habari za kimahakama zilithibitisha tarehe hiyo ya uamuzi.
Katika hoja zake za kutaka kesi hiyo itupiliwe mbali, Mughwai aliwaeleza majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu Othmani Chande kuwa kesi hiyo kuwa ni batili kwa kuwa imekosa vitu muhimu vya kisheria, ikiwamo tarehe ya rufaa hiyo kuandaliwa, kulalamikia kipengele ambacho hakijamtoa Lema madarakani pamoja na kutokuwa na muhuri wa Mahakama Kuu iliyoidhinisha rufaa hiyo.
Mughwai alisema katika nakala ya hati ya kukazia hukumu iliyowasilishwa mahakamani hapo, haina tarehe ya kuandaliwa kwake hali inayotia wasiwasi iwapo itakuwa imeandaliwa ndani ya kipindi kinachotakiwa kisheria cha siku 60 tangu kutolewa kwa hukumu au la.
Alidai mbali na nakala hiyo kukosa tarehe ya kuandaliwa kwake, pia haikuwa na muhuri wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuthibitisha kuwa ni kweli imetolewa na mahakama hiyo kwa kuwa nakala hiyo ilikuwa na saini tu ya Jaji Gabriel Rwakibarila ambayo haithibitishi uhalali wake.
Naye Wakili wa waomba rufaa, Method Kimomogoro akijibu hoja hizo, alikiri kuwa ni kweli nakala hiyo ina upungufu na ni makosa ya kibinadamu ambayo hata hivyo hayana athari katika kesi ya msingi hivyo aliwaomba majaji kutupilia mbali pingamizi hizo.
Aidha, Wakili wa Serikali, Timon Vitalis aliunga mkono hoja zilizotolewa na Wakili Kimomogoro huku akidai suala hilo la upungufu, lawama hazipaswi kuelekezwa kwa waomba rufani wala mawakili, bali zinapaswa kuelekezwa kwa mahakama ambayo ndiyo iliyoandaa hati hiyo.
Chanzo: http://www.wavuti.com/
Chadema kuchukua kata jimbo la Januari Makamba
Ni
ukweli usiopingika kwamba Mkoa wa Tanga ni ngome ngumu kwa CDM lakini
ukweli huu unakwenda kugeuka kuwa uongo.Kadri siku zinavyozidi kwenda ni
dhahiri kwamba upepo wa mabadiliko unazidi kushika kasi na ukweli huu
utaanza kudhihirika kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Tamota
Jimbo la Bumbuli.
Nimepata fursa ya kuzunguka jimbo la Bumbuli, jimbo la Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ndugu January Makamba na kujifunza mambo mengi tofauti na unavyoweza kumsikia na kumsoma kwenye magazeti, he deserve to be called Media Boy kwasababu hakubaliliki kwa namna ambavyo watu wengi wanaweza kufikiri zaidi ya kujenga jimbo kwenye magazeti na mitandao ya kijamii. Ukweli ni kwamba ni mwepesi mno silaha kubwa anayotumia ni nguvu ya fedha basi.
Kata ya Tamota ni moja kati ya kata 29 (moja ya kata mbili kwa Mkoa wa Tanga) nchi nzima ambapo kutakuwa na uchaguzi mdogo wa udiwani, kwa hali halisi ya kisiasa ilivyo ni dhahiri kwamba CHADEMA inakwenda kushinda na kuhesabu kata ya kwanza mkoa wa Tanga. Ni ukweli uliowazi kwamba ushindi wa kata hii utakuwa na maana kubwa kwa chama na hasa katika kueneza fikra za mabadiliko mkoa wa Tanga. Ni STAMINA Amir Sheshe anayetegemewa kutangazwa kuwa diwani wa kwanza wa CDM mkoa wa Tanga mnamo tarehe 28/10/2012.
Habari na Mbelwa Germano.
MAKAMANDA WA M4C (MAGOMA Jr MAGOMA-MWENYE KOMBATI YA KAKI, HENRY KILEWO-MWENYE KOMBATI NYEUSI, KAMANDA LEMA, M/KITI TANGA NA DIWANI MTARAJIWA KATA YA TAMOTA STAMINA- (MWENYE SUTI) WAKIWE KWENYE HARAKATI ZA KUSAMBARATISHA NGOME YA JANUARY MA KAMBA KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KATA YA TAMOTA, ILI KUFIKA KATA YA TAMOTA TULIPITA BARABARA YA VUMBI UMBALI WA KM 85 KUTOKA SONI (LUSHOTO), KISHA TUKATEMBEA KWA MIGUU KM 6 ILI KUFIKA KIJIJINI ALIKOZALIWA MZEE YUSUPH MAKAMBA
Nimepata fursa ya kuzunguka jimbo la Bumbuli, jimbo la Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ndugu January Makamba na kujifunza mambo mengi tofauti na unavyoweza kumsikia na kumsoma kwenye magazeti, he deserve to be called Media Boy kwasababu hakubaliliki kwa namna ambavyo watu wengi wanaweza kufikiri zaidi ya kujenga jimbo kwenye magazeti na mitandao ya kijamii. Ukweli ni kwamba ni mwepesi mno silaha kubwa anayotumia ni nguvu ya fedha basi.
Kata ya Tamota ni moja kati ya kata 29 (moja ya kata mbili kwa Mkoa wa Tanga) nchi nzima ambapo kutakuwa na uchaguzi mdogo wa udiwani, kwa hali halisi ya kisiasa ilivyo ni dhahiri kwamba CHADEMA inakwenda kushinda na kuhesabu kata ya kwanza mkoa wa Tanga. Ni ukweli uliowazi kwamba ushindi wa kata hii utakuwa na maana kubwa kwa chama na hasa katika kueneza fikra za mabadiliko mkoa wa Tanga. Ni STAMINA Amir Sheshe anayetegemewa kutangazwa kuwa diwani wa kwanza wa CDM mkoa wa Tanga mnamo tarehe 28/10/2012.
Habari na Mbelwa Germano.
MAKAMANDA WA M4C (MAGOMA Jr MAGOMA-MWENYE KOMBATI YA KAKI, HENRY KILEWO-MWENYE KOMBATI NYEUSI, KAMANDA LEMA, M/KITI TANGA NA DIWANI MTARAJIWA KATA YA TAMOTA STAMINA- (MWENYE SUTI) WAKIWE KWENYE HARAKATI ZA KUSAMBARATISHA NGOME YA JANUARY MA KAMBA KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KATA YA TAMOTA, ILI KUFIKA KATA YA TAMOTA TULIPITA BARABARA YA VUMBI UMBALI WA KM 85 KUTOKA SONI (LUSHOTO), KISHA TUKATEMBEA KWA MIGUU KM 6 ILI KUFIKA KIJIJINI ALIKOZALIWA MZEE YUSUPH MAKAMBA
Mnyika: Watendaji hawaelezi ukweli tatizo la umeme
WAZIRI
Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, ameeleza kusikitishwa na kauli
za viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la
Umeme nchini (TANESCO) kuhusu hali ya uzalishaji, usafirishaji na
usambazaji wa umeme nchini sanjari na uboreshaji wa utendaji TANESCO.
Amesema
kauli hizo zinatoa matumaini potofu kwa wananchi na kuwasihi kuzipokea
kwa tahadhari kwa kuwa hazielezi ukweli kuhusu tatizo la umeme nchini.
Mnyika
ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, alitoa kauli hiyo jana katika taarifa
yake kwa vyombo vya habari na kusema kulingana na nyaraka alizonazo za
ndani ya wizara hiyo na TANESCO kuanzia Septemba hadi Oktoba mwaka huu,
hali ya uzalishaji na usafirishaji na usambazaji wa umeme imekuwa tete
kwa sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa upatikanaji wa mafuta na gesi
asili kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya kufua umeme na kasi ndogo ya
uwekezaji kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa kudumu.
Mnyika pia
alisema amemwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, ili Wizara ya
Nishati na Madini iwajibike kueleza hali halisi katika mikutano ya
kamati za Bunge inayoendelea.
“Katika
barua hiyo nimependekeza pamoja na mambo mengine suala la kupokea na
kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na
utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa utendaji wa TANESCO
lishughulikiwe na kamati nyingine kwa haraka kwa kuzingatia maelezo na
maelekezo ya Spika aliyoyatoa bungeni wakati wa kuahirisha mkutano wa
nane wa Bunge,” alisema.
Aidha
alisema mapitio ya utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa utendaji wa
shirika hilo yahusishe kamati ya kudumu ya Bunge na itakayoeleza hatua
iliyofikiwa katika uchunguzi wa tuhuma za ufisadi kwa kuzingatia kuwa
siku 60 za uchunguzi zimepita.
Tanzania Daima
Sunday, October 21, 2012
CHADEMA yaeleza chanzo cha vurugu za Waislamu Dar
IMEELEZWA
kuwa vurugu za kikundi cha Waislamu zilizotokea Mbagala hivi karibuni ni
matokeo ya muda mrefu ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete kupuuzia kushughulikia matatizo yao.
Kauli hiyo
ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando na Profesa
Abdallah Safari, wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya
msimamo wa chama hicho dhidi ya vurugu za kidini zilizotikisa Jiji la
Dar es Salaam wiki hii.
Marando
alisema kuwakamata viongozi wa Kiislamu pasipo kushughulikia matatizo
yao si njia sahihi kwani kuna hatari ya kuzalisha Waislamu wengi wenye
msimamo mkali dhidi ya serikali na kuifanya nchi kutotawalika.
“Kabla ya
uhuru Waislamu walikuwa na taasisi zao serikali ya TANU, kwa ajili ya
kulinda masilahi yake ikavifutilia mbali na kuamua kuwawekea Waislamu
Bakwata na kutunga sheria za kuongoza, nataka mtambue matatizo ya
Waislamu wote hayasimamiwi na Bakwata, waitwe Waislamu na waulizwe shida
zao,” alisema Marando.
Aliongeza
kuwa kabla ya uhuru Waislamu walipambana kwa kuamini walikuwa
wakinyanyaswa na kwamba baada ya uhuru hawakuona mabadiliko yoyote,
hivyo wanalazimika kujitafutia uhuru mwingine mbali na ule wa kutoka
katika mikono ya wakoloni.
Alisema
serikali isisubiri vifo vitokee ndiyo ione umuhimu wa kushughulikia
matatizo hayo na badala yake ijipe muda wa kukaa na makundi yote
kutafuta muafaka.
“Siamini
kama kuna tatizo baina ya Waislamu na Wakristo bali mfumo wa serikali
unawalazimisha Waislamu kuamini hivyo kwa kuwa wametengwa, hawasikilizwi
hawathaminiwi na sasa wako kama yatima kwanini?” alihoji Marando.
Akizungumzia
utekwaji wa watu unaoendelea nchini, Marando alisema serikali haiwezi
kukwepa lawama hizo na kwamba matamshi ya viongozi wa Ikulu kuwa
hawamfahamu Ramadhani Ighondu ni hadaa kwa Watanzania.
“Sheikh
Farid alipotea katika mazingira ya ajabu na hili ni jukumu la serikali
kujua hatima ya raia wake lakini leo tunaona vyombo vya ulinzi vikisema
havihusiki wala havina habari na kupotea kwake, haya ni majibu kama yale
yale yaliyotolewa kwa Dk. Ulimboka,” aliongeza Marando.
Kwa upande
wake Profesa Safari alizungumzia kitendo cha Jeshi la Wananchi wa
Tanzania kuingilia kati kutuliza ghasia inaonesha kuwa serikali
imeshindwa kuongoza nchi kwa kufuata sheria.
“Jeshi la
Wananchi limefuata nini mtaani? Kuna tishio gani la amani
inayowalazimisha wao kuingia mtaani? Kwa kuwa tunafahamu suala la
kutangaza hali ya hatari na jeshi kuingia mtaani lazima liwe na baraka
ya Bunge,” alisema Safari.
Aliongeza
kuwa mara nyingi serikali imeshauriwa kutatua migogoro baina ya Waislamu
na serikali, lakini ushauri huo umekuwa ukipuuzwa.
Tanzania Daima
Saturday, October 20, 2012
Mfadhili wa CCM ajiunga na CHADEMA
Chadema jana ilifanya Mkutano wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.
Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.
Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.
Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.
Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.
Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.
Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi.
Friday, October 19, 2012
Tuesday, October 16, 2012
Mnyika kuwasha moto zuio la fao la kujitoa mifuko ya kijamii
MBUNGE
wa Ubungo (Chadema) John Mnyika amewasilisha kwenye ofisi za Bunge
kusudio la muswada binafsi wa kubadili sheria moja ya vipengele
vinavyosimamia kanuni za mafao kwa Taasisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
kuhusu kusimamishwa kwa fao la kujitoa.
Mnyika
aliwasilisha kusudio hilo kwa Katibu wa Bunge jijini Dar es Salaam jana
akisema amefanya hivyo baada ya kubaini Serikali iko usingizini licha ya
kuahidi kufanya marekebisho ya sheria hiyo.
Mbunge huyo
alieleza hayo jana kupitia taarifa yake kwa gazeti hili akisema
anatarajia kuwasilisha katika Bunge lijalo muswada binafsi wa sheria ya
Marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii kwa hati ya dharura
akizingatia kanuni ya 81 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la 2007.
“Lengo la Muswada huu ni kufanya marekebisho yenye kuboresha mfumo wa utoaji wa mafao nchini ikiwemo kuwezesha kutolewa kwa fao la kujitoa na mafao mengine muhimu ambayo hayatolewi katika utaratibu wa sasa wa mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii,” alisema Mnyika.
“Lengo la Muswada huu ni kufanya marekebisho yenye kuboresha mfumo wa utoaji wa mafao nchini ikiwemo kuwezesha kutolewa kwa fao la kujitoa na mafao mengine muhimu ambayo hayatolewi katika utaratibu wa sasa wa mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii,” alisema Mnyika.
Mnyika
alisema amefikia uamuzi huo kwa kuwa mpaka sasa zimebaki siku chache
Mkutano wa Tisa wa Bunge kuanza wakati Serikali imekaa kimya licha ya
kuahidi kuwa itapeleka marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii
Bungeni.
“Mpaka sasa Serikali haijaitisha mkutano na wafanyakazi pamoja na wadau wa jamii kupokea mapendekezo, hali ambayo inaashiria upo uwezekano muswada huo usiwasilishwe kwa wakati,” alisema Mnyika.
“Mpaka sasa Serikali haijaitisha mkutano na wafanyakazi pamoja na wadau wa jamii kupokea mapendekezo, hali ambayo inaashiria upo uwezekano muswada huo usiwasilishwe kwa wakati,” alisema Mnyika.
Taarifa hiyo
iliongeza kuwa kufutwa kwa mafao ya kujitoa msingi wake haupo kwenye
marekebisho ya sheria yaliyofanyika Aprili13 mwaka huu pekee bali ni
udhaifu katika mfumo mzima wa kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii
nchini, hali ambayo inahitaji wadau kutaka mabadiliko.
“Kufuatia
kuanza kutumika kwa Sheria hiyo (ya 13 Aprili 2012) maombi mapya ya
kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo
itakapotolewa ili kuwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa
elimu kwa wadau
Mwananchi
Monday, October 15, 2012
Mnyika: Spika aunde Kamati ya Gesi
WAZIRI
Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amemtaka Spika wa Bunge, Anna
Makinda, kutumia madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati
nyingine ya kudumu ya Bunge itakayoshughulikia masuala ya gesi asili
kabla na wakati wa mkutano wa Bunge ujao mwishoni mwa mwezi huu.
Mnyika
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, alisema hatua hiyo ni
kutokana na hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini
na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi
na maisha ya wananchi.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mnyika alisema pamoja na mambo
mengine, Spika Makinda aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili taarifa
ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu sekta ndogo ya
gesi asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma
za ufisadi.
Madai
mengine ni ya mapunjo ya fedha za mauzo ya gesi asili na hatua
iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi
asili.
“Hatua hii
ni muhimu kufuatia ukimya wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo kuhusu kauli yangu ya Oktoba 4, 2012 ya kutaka taarifa ya
ufafanuzi kuhusu utafutaji wa mafuta na gesi asili nchini iliyotolewa na
wizara hiyo Septemba 21 mwaka huu ifutwe,” alisema.
Alisema kuwa
taarifa hiyo ya wizara ilieleza kuwa maandalizi ya sera ya gesi asili
yapo katika hatua za mwisho wakati ambapo kamati mbalimbali za kudumu za
Bunge hazijahusishwa katika mchakato huo muhimu pamoja na kuwa mamlaka
ya kutunga sera kwa mfumo wa sasa ni ya Baraza la Mawaziri.
“Kwa unyeti
na upekee wake sera ya gesi, Spika wa Bunge anapaswa kuwezesha Kamati za
Kudumu za Bunge zihusishwe ili pawepo mashauriano na maridhiano kwa
mapana na marefu,” alisema.
Mnyika
alisema izingatiwe kwamba katika mkutano wa nane wa Bunge, Spika
alitangaza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imevunjwa
na kwamba majukumu iliyokuwa ikishughulikiwa yatashughulikiwa na kamati
nyingine kwa mujibu wa madaraka na mamlaka ya spika.
Tanzania Daima
Sunday, October 14, 2012
Saturday, October 13, 2012
Viongozi CHADEMA wanasurika kutekwa
VIONGOZI wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamenusurika kutekwa baada
ya gari lao aina ya Toyota Opa lenye namba za usajili T 850 BLK,
kushambuliwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa kioo cha nyuma na kitu
kizito.
Tukio hilo
lilitokea Oktoba 9, mwaka huu majira ya saa nne usiku wakati viongozi
hao wakitoka katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa
madiwani katika Kata ya Mpwapwa Mjini.
Shambulizi
dhidi ya viongozi hao waliokuwa katika gari hilo mali ya Eva Mpagama
ambaye ni Mratibu wa Vijana CHADEMA Mkoa wa Dodoma, lilifanyika katika
eneo la Mwanakianga, nje kidogo ya mji wa Mpwapwa.
Walioshambuliwa
ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo CHADEMA Taifa, Benson
Kigaila, Mratibu wa Vijana Mkoa wa Dodoma, Mpagama na Kunti Yusufu
ambaye ni mratibu wa akina mama CHADEMA mkoa.
Tukio hilo liliripotiwa Oktoba 10 katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpwapwa, na kufunguliwa jalada namba RB/1934/2012.
Tanzania Daima
Friday, October 12, 2012
CHADEMA kujadili ripoti za Mwangosi
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kinakusudia kufikisha ripoti za kamati mbalimbali zilizochunguza mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha television cha Chanel Ten katika kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa ajili ya hatua zaidi.
Hata hivyo, mbali ya hatua hiyo, chama hicho kimesisitiza kuwa ni wakati muafaka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emanuel Nchimbi, kuachia nafasi au awajibishwe na Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kutumia fedha za wananchi kwa kamati waliyodai haikuwa na jipya juu ya mauaji ya Mwangosi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri Kivuli wa Wizara hiyo, Vicent Nyerere, alisema wao kama chama wameona watoe tamko la awali wakati wakisubiri majumuisho ya pamoja kwa ajili ya hatua zaidi.
“Serikali toka awali haikuwa na nia ya kuonesha upungufu uliosababisha kifo cha Mwangosi, na kwa kutambua hili Nchimbi aliunda kamati yenye lengo la kuisafisha jeshi la Polisi kwa kutumia kodi zetu,”alisema.
Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, aliongeza kuwa ni jambo la ajabu kwa mtu kama Nchimbi kukubali kupokea ripoti ya ajabu na yenye kumdhalilisha kisha akasimama hadharani kuitetea.
Alisema ni wakati muafaka kwa Rais Kikwete kumfuta kazi Dk. Nchimbi kwa kuwa ameshindwa kujitathmini kutokana na mauaji yanayotokea sehemu mbalimbali hasa katika matukio ya kisiasa ili liwe fundisho kwa viongozi wengine katika kusimamia majukumu na maslahi ya Taifa.
Nyerere alibainisha kuwa namna kamati ya Dk. Nchimbi ilivyofanya kazi, imeshindwa kuwaelewesha watanzania kiini cha kifo hicho licha ya kutumia kodi zao, hivyo kushauri kuwa inapaswa kuundwa tume ya kimahakama.
Kuhusu maoni ya kamati ya Dk. Nchimbi juu ya shughuli za kisiasa kuishia bungeni baada ya uchaguzi, Nyerere alisema ni jambo la kushangaza kama leo Bunge litakuwa sehemu ya kunadi sera badala ya kuzungumzia matatizo ya wananchi.
“Kama kamati iliyo chini ya Jaji Ihema ndiyo imekuja na mtazamo huu wa kutaka shughuli za kisiasa na mijadala yake ifanyikie bungeni basi ninasisitiza kauli ya Tundu Lissu juu ya kumpinga Jaji huyu mstaafu ni muhimu zaidi,”aliongeza Nyerere.
Alisema ripoti ya kamati ya Nchimbi ingeweza kutoa taarifa zote hadharani bila kuingilia uhuru wa mahakama na kwamba alitaraji kuona ikiwagusa viongozi wa serikali moja kwa moja wanaoingilia shughuli za vyama vya siasa.
Kamati tatu tofauti zimetoa ripoti zake kuhusiana na mauji ya Mwangozi ambapo ile ya Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri pamoja na ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, zimeeleza wazi kiini cha mauji hayo na kuwataja waliohusika.
Hata hivyo ripoti ya kamati iliyoundwa na Waziri Nchimbi ililalamikiwa kutokana na kushindwa kuweka taarifa kamili wazi kwa madai kuwa kesi ya mauaji hayo iko mahakamani.
Tanzania Daima
Thursday, October 11, 2012
Mbowe awaonya polisi
MWENYEKITI
wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe,
amelionya Jeshi la Polisi akisema haliwezi kuzima vuguvugu la mabadiliko
(M4C) nchini kwa kutumia risasi kutisha na kuua wananchi.
Badala yake,
amelitaka kufanya shughuli zake kwa utaalamu kwa kuzingatia sheria na
kanuni zinazolisimamia na kuepuka kutumiwa kutekeleza matakwa ya
watawala wanaowaagiza kuwanyanyasa wapinzani.
Mbowe alitoa
onyo hilo juzi wakati akimnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Daraja
mbili, Prosper Msofe katika Mtaa wa Jamhuri, ambaye hata hivyo hakuweza
kuhudhuria mkutano huo kutokana na kulazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru akipatiwa matibabu ya uti wa mgongo baada ya kushikiliwa na polisi.
Licha ya
mgombea huyo kutokuwepo mkutanoni, Mbowe alimtaka kutotishika na tukio
lililompata badala yake iwe changamoto ya kuzidi kudai na kupigania haki
kwa maslahi ya umma.
“Kama sababu
ya CHADEMA kuitwa chama cha vurugu ni kwa kutokana na hatua yetu ya
kuwahamasisha watu kudai na kupigania haki zao, basi acha tuendelee
kutambulika hivyo,” alisema.
Mbowe
alieleza kushangazwa na hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kushindwa kutangaza uchaguzi katika kata nne za Jiji la Arusha ambazo
zilikuwa zinaongozwa na madiwani waliotimuliwa CHADEMA tangu mwaka jana
licha ya juhudi walizofanya kuikumbusha kwa maandishi.
Kata hizo ni
Elerai, Kimandolu, Kaloleni, Themi na Sombetini iliyokuwa ikishikiliwa
na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia aliyekuwa diwani wake, Alphonce
Mawazo, ambaye alijivua gamba kwa kujiunga na CHADEMA.
“Woga wao
wanajua nguvu ya CHADEMA kwa sasa, wanaogopa kuona tukishinda viti hivi
na kuingiza madiwani sita pamoja na wa viti maalum, idadi ya madiwani
wetu itakuwa kubwa, hivyo tutaongoza Halmashauri ya Jiji la Arusha,”
alisema.
Akizungumzia
utaratibu wa CHADEMA kuwachangisha wanachama wake fedha kwenye mikutano
yao kwa ajili ya kuchangia gharama za uendeshaji, alisema kuwa chama
kinajengwa na watu wenye fedha safi kama hizo.
Naye Mjumbe
wa Baraza Kuu Taifa wa CHADEMA, Godbless Lema, aliwataka polisi wadogo
kutokubali kutumiwa kutekeleza amri za kikandamizaji za viongozi wao
kuumiza wananchi kwani mwisho wa siku watakaohukumiwa ni wao.
Alisema kuwa
kwenye vurugu za Arusha za Januari 5 mwaka jana, walikufa watu watatu
ambapo polisi wa vyeo vya juu ndio walioongezewa vyeo huku wale wa chini
wakiambulia patupu.
Tanzania Daima
Wednesday, October 10, 2012
Mgombea udiwani CHADEMA alazwa
MGOMBEA
udiwani kata ya Daraja Mbili kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo, (CHADEMA), Prosper Msofe, amelazwa kwenye hospitali ya mkoa
ya Mount Meru akisumbuliwa na maumivu ya uti wa mgongo baada ya
kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi cha kati, Arusha usiku wa juzi kuamkia
jana.
Katibu wa
wilaya ya Arusha wa CHADEMA, Martin Sarungi, na aliyekuwa mbunge wa
Arusha, Godbless Lema, waliwaeleza waandishi wa habari mbele ya kituo
cha polisi kuwa mgombea wao alikamatwa majira ya saa mbili usiku eneo la
Friends Corner baada ya kuhoji sababu wamachinga kunyang’anywa bidhaa
zao na Ramadhan Kalamba (56) anayedai kuwa halmashauri ya jiji imempa
jukumu la kuwaondoa machinga katikati ya jiji.
“Msofe
alihoji sababu za Ramadhan kuchukua mali za wamachinga majira ya usiku
wakati ambao halmashauri haifanyi kazi; alikuwa akizipeleka wapi na ni
nani aliyempa mamlaka ya kuchukua vitu hivyo ndipo gari la polisi
likafika na kumchukua,” alisema Lema.
Walisema
kuwa baada ya kupata taarifa za mgombea wao huyo kukamatwa, baadhi ya
wanachama na viongozi walimfuatilia mpaka kituo cha polisi kwa lengo la
kumwekea dhamana jambo ambalo lilishindikana ndipo majira ya saa nne
usiku wakaamua kuondoka.
Hata hivyo
Kamanda wa Polisi mkoani hapa (RPC), Liberatus Sabas, alikanusha madai
hayo kwa kile alichoeleza kuwa mgombea huyo hakunyimwa bali alikataa
dhamana mwenyewe ambapo alidai kuwa alikamatwa na askari wa doria na
kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumpiga ngumi ya kifuani Kalamba.
Alisema kuwa
jeshi la polisi lilipata taarifa kuwa Kalamba anashambuliwa ndipo
askari wa doria walipofika na kumchukua Msofe ambapo alisema kuwa mzozo
baina ya wawili hao ulitokana na hatua ya Msofe kuhoji sababu za Kalamba
kutaka wamichinga hao waondoke eneo hilo huku akijaribu kumzuia
asiendelee kutangaza.
Awali jana
majira ya saa nne asubuhi mgombea huyo wa CHADEMA alienda kupatiwa
matibabu kwenye zahanati ya polisi akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi
la polisi ambapo daktari wa zahanati hiyo alishauri apelekwe hospitali
ya mkoa kwa uchunguzi zaidi lakini polisi waliamua kumpeleka mahakama ya
mwanzo ya Maromboso.
Baadhi ya
viongozi wa CHADEMA waliokuwa mahakamani hapo walikwenda kuuona uongozi
wa mahakama na kuwaonyesha cheti alichopatiwa mtuhumiwa huyo
kinachomtaka apelekwe hospitali ya mkoa kwa uchunguzi zaidi jambo ambalo
linadaiwa pengine ndilo lililopelekea mtuhumiwa huyo kutofikishwa mbele
ya hakimu.
Mgombea huyo
ambaye alikuwa amepakiwa kwenye gari ya polisi yenye namba za usajili
PT 1844 ambayo ubavuni imeandikwa OCD Arusha alikaa rumande ya mahakama
hiyo kwa zaidi ya saa moja ambapo gari hilo lilirudi likiwa limeongeza
idadi ya askari wenye silaha wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hii
(OCD), G. A Muroto na kumchukua ambapo walimpeleka moja kwa moja
hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
Wagombea
wengine katika kinyang’anyiro hicho na vyama vyao kwenye mabano ni
Philip Philip (CCM), Mohamed Msuya (NCCR-Mageuzi), William Laizer (TLP)
na Zani Zakaria (CUF).
Tanzania Daima
Tuesday, October 9, 2012
Chadema yaibana Polisi kutoroka kwa watuhumiwa wa mauaji
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelitaka Jeshi la Polisi kutoa
maelezo ya kutosha yatakayoendana na uwajibikaji na hatua za kisheria,
kufuatia watuhumiwa wawili wa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama
hicho, Kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo, kutoroka mbele ya askari
wenye silaha.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko kitendo cha watuhumiwa hao kutoroka mbele ya askari wenye silaha, baada ya kumnyang’anya bunduki mmoja wa askari waliokuwa lindo eneo la mahakama ya wilaya.
Alisema Chadema inasikitika kwa kitendo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kugoma kutaja jina la askari aliyenyang’anywa bunduki na hata majina ya wenzake waliokuwa lindo mahakamani.
Alisema kutokana na tukio hilo lenye utata, kuna umuhimu wa kuundwa kwa chombo huru cha uchunguzi wa mauaji yenye utata, yanayohusishwa na siasa, mojawapo likiwa ni tukio la mauaji ya Mbwambo.
Lwakatare alisema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katika barua aliyomwandikia Rais, alimtaka kuunda Tume ya Kijaji/ Kimahakama ya uchunguzi wa vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yaliyohusisha Chadema.
“Ni bahati mbaya kuwa wakati Watanzania wapenda haki wakisubiri kujua majibu ya Rais kwa barua hiyo, masuala kadhaa yametokea, ambayo yote yameonesha kuwa serikali ya CCM inazidi kukomaza mfumo wa kulindana na kutaka kuficha masuala fulani fulani, hasa katika matendo ya mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi,”alisema Lwakatare.
NIPASHE
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko kitendo cha watuhumiwa hao kutoroka mbele ya askari wenye silaha, baada ya kumnyang’anya bunduki mmoja wa askari waliokuwa lindo eneo la mahakama ya wilaya.
Alisema Chadema inasikitika kwa kitendo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kugoma kutaja jina la askari aliyenyang’anywa bunduki na hata majina ya wenzake waliokuwa lindo mahakamani.
Alisema kutokana na tukio hilo lenye utata, kuna umuhimu wa kuundwa kwa chombo huru cha uchunguzi wa mauaji yenye utata, yanayohusishwa na siasa, mojawapo likiwa ni tukio la mauaji ya Mbwambo.
Lwakatare alisema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katika barua aliyomwandikia Rais, alimtaka kuunda Tume ya Kijaji/ Kimahakama ya uchunguzi wa vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yaliyohusisha Chadema.
“Ni bahati mbaya kuwa wakati Watanzania wapenda haki wakisubiri kujua majibu ya Rais kwa barua hiyo, masuala kadhaa yametokea, ambayo yote yameonesha kuwa serikali ya CCM inazidi kukomaza mfumo wa kulindana na kutaka kuficha masuala fulani fulani, hasa katika matendo ya mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi,”alisema Lwakatare.
NIPASHE
CHADEMA waahidi makubwa
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Mvomero, kimezindua kampeni
ya udiwani wa Kata ya Mtibwa kwa ahadi mbalimbali ikiwemo kudai chenji
ya fedha za mfuko wa jimbo kwa Naibu Waziri wa Utamaduni na Michezo na
Mbunge wa jimbo hilo, Amos Makala, zinazodaiwa kutofanya kazi tangu
mwaka 2010.
Uzinduzi huo
uliofanyika kwenye uwanja wa Kambombe Madizini B, ulihudhuliwa na
viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya za jirani,
ulizinduliwa na Mwenyekiti wa Madiwani wa chama hicho mkoani hapa ambaye
pia ni diwani wa Gairo, Dastan Mwendi.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo, Mwendi alisema: “Uoga na vitisho vya nguvu za dola
ikiwemo kuua kwa makusudi raia nchini umetufikisha kwenye dimbwi la
umasikini wa kutupwa tulio wengi na kuwanufaisha wachache walioko
madarakani…wakati tunauawa na watoto kukosa elimu yenye tija inayotokana
na kukosa huduma na vifaa wenzenu wananepa. Mchagueni Lucas
Mwakambaya,” alisema huku akihoji zilipo fedha za jimbo tangu mwaka
2010”.
Akiwahimiza
wapiga kura kumchagua Mwakambaya kuwa diwani wa Kata ya Mtibwa, Mwendi
alisema muda wa Watanzania kugeuzwa ‘kuku wa kienyeji’ na kuwa wenye
thamani wakati wa matatizo na furaha umepitwa na wakati kwa kuwa sasa
wanaelewa haki zao.
Mwenyekiti
wa chama hicho wa manispaa, Zuberi Kiloko na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa,
Boniface Ngonyani, waliungana na hoja hizo kwa nyakati tofauti na kusema
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeelemewa na uongozi mbovu uliojaa rushwa
na uonevu kwa wanachi.
“Chama
makini huonekana hata katika uendeshaji wa michakato midogomidogo ya
kichama, leo hii CCM inanuka rushwa hadi mwenyekiti wao Jakaya Kikwete
amewashitukia na kutoa tamko kali kuwa atakayebainika kutoa rushwa
atafutiwa uanachama, hii inatokana na kukithiri kwa rushwa,” alisema
Kiloko.
Akijinadi
mgombea udiwani wa Mtibwa, Mwakambaya, alitaja changamoto tisa
zinazomkosesha usingizi na anazokusudia kuzifuatilia na kuzisimamia
kikamilifu ikiwemo ya wenyeviti wa vijiji na vitongoji kutosoma taarifa
za mapato na matumizi, upotevu wa sh milioni 28 kila mwezi na
kutelekezwa kwa mnada miaka nane bila kuboreshwa huduma za kijamii.
Changamoto
nyingine ni dhuluma zinazofanywa na kiwanda wa sukari cha Mtibwa ikiwemo
ya kutolipa mafao ya wastaafu kwa miaka minane na fidia kwa
waliohamishwa kupisha Sekondari ya Mtibwa, tatizo la ukosefu wa
zahanati, soko, kuifuta michango isiyo na tija na kuikagua upya miradi
yote iliyopo katani hapo.
Tanzania Daima
Mnyika: CCM ni janga
MBUNGE wa
Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amewataka Watanzania kukichukulia Chama
cha Mapinduzi (CCM) na kukiona kama janga la kitaifa kwani kimeshindwa
kutatua matatizo yao.
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Msalato, manispaa ya Dodoma.
Mnyika
alisena kuwa CCM imechangia kwa kiasi kikubwa kuwadidimiza Watanzania
kutokana na kushindwa kusimamaia rasilimali zilizopo na kuwaruhusu
wageni kuzitumia bila kuwashirikisha Watanzania.
Alisema kuwa
Watanzania wengi wamekuwa maskini katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru
wakati kuna wachache ambao wanamiliki fedha nyingi.
CHADEMA wamemsimamisha Nsubi Bukuku kuwa mgombea udiwani katika kata hiyo.
Naye Afisa
Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, alisema vurugu zilizotokea juzi kabla
ya mkutano wao juzi zilisababishwa na wanachama wa CCM kuvamia msafara
wao.
Majeruhi
katika vurugu hizo ni Katibu wa UVCCM wa kata ya Kiwanja cha Ndege, Ali
Swalehe; mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa CCM Dodoma Mjini, Fatma
Mwihidini; Diwani wa kata ya Uhuru, Ali Kimaro; Hussein Mtengule na
Waziri Shabani.
Hata hivyo, habari hizo zilisema kuwa hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi kuhusiana tukio hilo hadi sasa.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa, Stephen Zelothe, alipoulizwa kuhusiana na vurugu
hizo alisema yuko safarini kurejea mjini Dodoma na kwamba angetoa
taarifa kwa waandishi atakapofika.
Tanzania Daima
CHADEMA yazindua kampeni za udiwani
UMATI mkubwa
wa watu, juzi ulijitokeza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za
mgombea udiwani wa kata ya Daraja Mbili wa Chama Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Prosper Msofe, uliofanyika kwenye mtaa wa Narvoi.
Aidha,
viongozi wa chama hicho wakizungumza katika mkutano huo mbali ya
kumuombea kura mgombea wao huyo, walitumia fursa hiyo kuutaka uongozi wa
jiji la Arusha kuacha kufuata shinikizo la kisiasa katika kutafutia
ufumbuzi suala la wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kwa
madai kuwa suala hilo ni kama bomu la muda linalosubiri kulipuka.
Pia
waliitaka serikali kutoa majibu yanayoeleweka juu ya tukio la kutoroka
kwa washtakiwa wawili wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa
CHADEMA, kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo, kwa madai kuwa kuna
uwezekano nyuma ya mpango huo, kukawa na mkono wa wanasiasa ambao
hawataki ukweli ujulikane.
Mwenyekiti
wa wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema inashangaza kuona
halmashauri ya jiji la Arusha inaamua kuendesha shughuli zake kijima kwa
kuamua kugawa uwanja wa NMC.
Nanyaro
ambaye pia ni diwani wa Levelosi, aliuataka uongozi wa jiji la Arusha
kushughulikia masuala yote kitaalamu kuepuka kuibua migogoro isiyo ya
lazima kama ilivyo sasa ambapo licha ya machinga kupewa eneo
lisilotosheleza kwenye uwanja wa NMC, lakini idadi ya waliokosa ni kubwa
hivyo badala ya tatizo kupungua limeendelea kuongezeka.
Kwa upande
wake, aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alisema serikali
isifanyie mzaha suala la watuhumiwa hao kutoroka, kwani lina utata
mkubwa na pia linaacha maswali mengi kuliko majibu.
Kampeni hizo zinatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 28, mwaka huu ambapo zinawashirikisha wagombea kutoka vyama vya CCM na TLP.
Tanzania Daima
CCM yaanguka tena
SASA UCHAGUZI MDOGO WANUKIA SUMBAWANGA
KWA mara
nyingine tena, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimegonga mwamba baada ya
Mahakama ya Rufaa Tanzania, kuitupilia mbali rufaa ya aliyekuwa Mbunge
wake wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly, aliyevuliwa ubunge na Mahakama
Kuu Kanda ya Sumbawanga Aprili 30, mwaka huu.
Uamuzi wa
kuitupilia mbali rufaa hiyo, umetolewa na jopo la majaji watatu, Januari
Msoffe, Edward Rutakangwa na Engela Kileo, baada ya kubaini kasoro za
kisheria.
Hilaly
alivuliwa ubunge na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Sumbawanga, Bethuel Mmila, kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa
mgombea ubunge kupitia CHADEMA, Nobert Yamsebo.
Hata hivyo,
Mei 28 mwaka huu, Hilaly alikata rufaa namba 55 ya mwaka 2012, dhidi ya
Yamsebo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Justus Kalama na Vitus
Kapufi, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu.
Rufaa hiyo
imebainika kuwa na dosari kadhaa ambazo zimeishawishi Mahakama ya Rufaa
Tanzania chini ya jopo la majaji hao kuitupilia mbali jana katika uamuzi
uliotolewa jijini Dar es Salaam.
Dosari hiyo
ni kutokuwepo kwa mwenendo wa maombi ya mlalamikaji katika kesi ya
msingi ya kuomba mahakama impangie kiwango cha fedha ambacho alipaswa
kulipa kama amana ya kufungua kesi hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 111
(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
Katika
uamuzi wake uliosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra
Maruma, mahakama hiyo ilirejea kifungu cha 111 (3) cha Sheria hiyo ya
Uchaguzi.
Kwa mujibu
wa kifungu hicho, Mahakama ilisema kwamba mtu anayefungua kesi ya
uchaguzi, ni lazima awasilishe maombi ili mahakama impangie kiwango cha
amana anachopaswa kulipa ndani ya siku 14 tangu kufungua kesi na kwamba
ndani ya siku 14 nyingine tangu siku ya maombi hayo, mahakama hiyo iwe
imeshapanga kiwango hicho.
Majaji hao
waliongeza kuwa, ni muhimu kwa sababu kuu mbili, moja ni kuipa nafasi
mahakama kuona kama maombi yaliwasilishwa ndani ya muda baada ya kesi
kufunguliwa na pili kuona kama maombi hayo yaliamuliwa ndani ya muda
tangu kuwasilishwa.
Kwamba kwa
mujibu wa Kanuni ya 96 (1) na (3) za Kanuni za Mahakama ya Rufani, si
jukumu la upande katika kesi kuamua kuwa nyaraka fulani ni muhimu au si
muhimu katika rufaa, kama wakili wa Hilaly, Rweyongeza alivyodai.
Mbali ya
kanuni hiyo, Mahakama hiyo pia ilirejea katika uamuzi wake katika rufaa
namba 8 ya mwaka 2008, Fedha Fund Limited na wenzake wawili, dhdi ya
George T.Varghese, pamoja na tafsiri ya Kanuni ya 85 (3) ya Kanuni za
Mahakama ya Rufani ya Kenya za mwaka 1979.
"Kutokana na
sababu hizo tulizokwisha kuzieleza hapo juu, tanarudia kusema kwamba
kumbukumbu zinazohusiana na mwenendo wa maombi ya kupangiwa kiwango cha
kulipa kama amana ni nyaraka muhimu katika rufaa.
Kutokuwepo
kwa nyaraka hizo, rufaa haina nguvu chini ya Kanuni ya 96 (1) (k) ya
Kanuni za Mahakama ya Rufani, hivyo rufaa inatupiliwa mbali," lilisema
jopo hilo.
Hata hivyo,
mahakama hiyo ilisema kuwa haiwezi kuamua upande wa warufani ulipe
gharama za rufaa hiyo kwa kuwa kasoro zilizosababisha kutupiliwa mbali
kwa rufaa hiyo ziliibuliwa na mahakama yenyewe.
Julai 3,
2012, AG na Kalama, nao walikata rufaa namba 65 ya mwaka 2012 dhidi ya
Yamsebo wakipinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.
Kutokana na
rufaa hizo dhidi yake, Yamsebo kupitia kwa Wakili wake Victor Mkumbe,
aliweka pingamizi la awali (PO) pamoja na mambo mengine akidai kuwa
Hilaly hakuwa amelipia ada ya kufungua rufaa hiyo ya Sh 2000.
Hata hivyo,
siku ambayo Mahakama ya Rufani ilipanga kusikiliza rufaa hiyo, iliamua
kuziunganisha rufaa hizo mbili, ambapo Hilaly aliunganishwa na AG pamoja
na Kalama wakawa waomba rufaa dhidi ya Yamsebo.
Kabla ya
kuanza kusikiliza pingamizi la Yamsebo dhidi ya rufaa ya Hilaly,
mahakama hiyo ilibaini kutokuwepo kwa mwenendo huo wa maombi ya Yamsebo
kupangiwa gharama za kufungulia kesi hiyo ya msingi.
Kutokana na kasoro hiyo, mahakama ilihoji na kutaka maoni ya mawakili wa pande zote kuhusiana na kasoro hizo.
Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Mwema Punzi alijibu kuwa wao walimwandikia barua
Msajili wa Mahakama ya Rufani Kanda ya Sumbawanga kumuomba mwenendo wa
kesi hiyo pamoja na vielelezo vingine na kwamba walipopewa, mwenendo wa
maombi ya gharama za kesi haukuwemo.
Wakili wa
Yamsebo, Mkumbe, alidai kuwa kutokana na kutokuwepo kwa mwenendo huo,
kunaifanya rufaa hiyo iwe batili, na akaiomba mahkama hiyo iitupilie
mbali.
Hata hivyo
Wakili wa Hilaly, Richard Rweyongeza, alidai kuwa kukosekana kwa
mwenendo huo hakuwezi kuifanya rufaa hiyo iwe ni batili, badala yake
aliiomba mahakama hiyo itumie mamlaka yake chini ya Kanuni ya 2 ya
Kanuni za Mahakama ya Rufani, ili iweze kuendelea.
Wakili
Rweyongeza aliongeza kwamba hata ikibainika kuwa hizo gharama za
kufunulia kesi hazikulipwa, anayeathirika ni mjibu rufaa, hoja ambayo
iliungwa mkono na Wakili wa Serikali, Punzi.
Katika kesi
hiyo ya msingi namba 01 ya mwaka 2010, Yamsebo alikuwa akipinga ushindi
wa Hilaly, akidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa Katiba na Sheria ya
Uchaguzi na hivyo kusababisha uchaguzi huo kutofanyika kwa haki na
uhuru.
Pia, alikuwa akimtuhumu Hilaly na wafuasi wake kutoa rushwa kwa wapiga kura mbalimbali ili wamchague.
Tuhuma
nyingine alikuwa akizieleka kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuwa alibadilisha
baadhi ya vituo vya kupigia kura kupelekwa mbali zaidi kati ya kilomita
tano hadi nane, jambo ambalo ilichangia kuathiri matokeo ya uchaguzi
huo.
Katika
uamuzi wake, Mahakama Kuu ilikubaliana na baadhi ya hoja zilizotolewa na
mlalamikaji na hatimaye kutengua ushindi wa Hilaly.
Akisoma
hukumu hiyo, Jaji Mfawidhi Betwell Mmila, alisema kuwa baada ya kupitia
hoja zote, anashawishika kusema kuwa uchaguzi katika jimbo hilo ulikuwa
si wa haki na huru.
Jaji Mmila
alieleza kuridhika kuwa kulikwepo na mazingira ya rushwa na kutokuwapo
kwa mazingira huru katika kampeni kwa baadhi ya maeneo.
Katika uchaguzi huo, Hilaly alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 17,328, huku Yamsebo akipata kura 17,132.
Kwa uamuzi
huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), itapaswa kuitisha upya uchaguzi
ndani ya siku 90 ikiwa Hilaly hatakata tena rufaa kupinga uamuzi huo
wa jipo la majaji hao.
wa jipo la majaji hao.
Tanzania Daima
Monday, October 8, 2012
CHADEMA yashinda rufaa Sumbawanga Mjini
Chama
cha CHADEMA kimeshinda rufaa iliyokatwa na aliyekua mbunge wa
SUMBAWANGA MJINI BW. AESH HILALY (CCM). Baada ya Rufaa hiyo kutupwa na
hivyo kutoa fursa ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo.
Habari kamili itawajia baadae.
Habari kamili itawajia baadae.
Mlinzi wa Mbowe azua balaa CCM
MLINZI
binafsi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe, amezua balaa kubwa kwa Chama cha Mapinduzi mkoani Arusha
kutokana na sura yake kufafanishwa na ile ya Mwenyekiti wa Umoja wa
Vijana (UVCCM) wilayani Arumeru, Boniface Mangaya Laizer, na hivyo
kusimamishwa uongozi.
Laizer
ambaye ni rafiki mkubwa wa kada wa CHADEMA mkoani Arusha, Ally Bananga,
aliyejiengua CCM mapema mwaka huu, amedaiwa kuonekana kwenye picha
gazetini akiwa na viongozi wa CHADEMA wakati wa operesheni ya chama
hicho katika mikoa ya kusini hivi karibuni.
Akizungumza
na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Boniface alisema kuwa ameshangazwa
na tuhuma hizo alizoziita kuwa ni mizengwe akidai kwamba hata huyo
mlinzi wa Mbowe, Zakaria Swai, anayefafanishwa naye hamfahamu.
“Mimi
sijawahi kuhudhuria mkutano wowote wa CHADEMA katika mikoa ya kusini na
tuhuma hizo zilipoibuliwa nikalazimika kumtafuta huyo mlinzi ili
nimfahamu. Katika picha iliyochapwa na gazeti moja la kila siku la Juni
mosi mwaka huu, anaonekana Bananga akiwa na Mbowe na viongozi wengine na
mlinzi huyo akiwa nyuma amevalia mawani meusi, sasa huyo
watamfananishaje na mimi na kunisimamisha?” alisema.
Katika barua
ya kujulishwa kusimamishwa kwake yenye kumb. Na. CM/AR/S/K. 13/3/Vol.
V/233 ya Oktoba mosi, mwaka huu, ikiwa imeandikwa na Katibu wa CCM Mkoa
wa Arusha, Mary Chatanda, mwenyekiti huyo anajulishwa kuwa anasimamishwa
kutokana na tuhuma za usaliti.
“ Tuhuma
zinazokukabili za kiitikadi na usaliti ni nzito ambazo zinakuondolea
sifa za kuwa kiongozi. Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Mkoa
iliyokutana kuanzia Septemba 27-29, mwaka huu, ilitafakari kwa kina
tuhuma zinazokukabili na kwa Mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya
CCM ya 1977 Toleo la 2007- Ibara ya 96 (7) iliazimia kukusimamisha
uongozi,” ilisomeka barua hiyo.
Chatanda
katika barua hiyo anaongeza kuwa Boniface anajulishwa rasmi kwamba
kuanzia sasa amesimamishwa uongozi hadi hapo mamlaka yenye uwezo juu
yake ya kikatiba itakapoamua vinginevyo.
Hata hivyo,
Boniface ambaye ameibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi uliomalizika
hivi karibuni, alisema kuwa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa UVCCM
wilayani humo kwa taratibu zote za chama na hivyo akashangaa uamuzi huo
umetoka wapi.
Alisema kuwa
wapiga kura wake pia wameshangazwa na uamuzi huo aliodai kuwa ni
mkakati wa viongozi wa mkoa kupandikiza kiongozi wanayemtaka wao awe
mwenyekiti wa UVCCM wilayani Arumeru.
Naye rafiki
yake wa karibu, Bananga, alizungumzia sakata hilo akisema huo ni
ushuhuda tosha kuwa Chatanda baada ya kumaliza kutimiza azma yake ya
kuvuruga vyama vya upinzani mkoani humo sasa dhambi hiyo imemrudia na
kuanza kukibomoa chama chake.
“Mimi
Boniface ni rafiki yangu wa karibu tangu nikiwa CCM hadi sasa, ila
kutokana na CCM kutapatapa na makundi yao Arusha wanadhani ninamtumia
kama pandikizi kuwabomoa. Anayeonekana kwenye ile picha si Boniface bali
ni Swai mlinzi wa Mbowe,” alisema.
Bananga
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha na Mjumbe wa Mkutano
Mkuu Taifa kupitia mkoa huo, aliongeza kuwa Chatanda ni janga la
kitaifa kwani amevuruga upinzani Arusha na sasa amegeukia chama chake.
Mwananchi