Chumba cha darasa ambacho mara nyingi nakitumia kufanya mitihani. Panaitwa NE 1.
Tuesday, July 26, 2011
IGUNGA Kumekucha.
LIPUMBA, SLAA WATAMBA KULINYAKUA JIMBO LA IGUNGA CCM BADO KIMYA
Waandishi wetu
SIKU chache baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutangaza kuwa kiti cha Jimbo la Igunga liko wazi kufuatia kujiuzulu kwa Rostam Aziz, vyama vya siasa vimeanza mbio za kuwania jimbo hilo.Rostam alijiuzulu ubunge wa Igunga Julai 13 mwaka huu, kutokana na kile alichokiita siasa uchwara ndani ya CCM, na wiki iliyopita Spika Makinda, alitangaza kuindikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuieleza kuwa kiti hicho cha ubunge, sasa kiko wazi.
Hatua ya Spika Makinda kuijulisha Nec kuhusu kujiuzulu kwa Rostam, ni mwanzo wa mchakato wa kukijaza kiti hicho cha ubunge kilichokuwa kikikaliwa na kada huyo wa CCM kwa miaka 18 iliyopita.Baada ya taarifa hiyo ya Spika Makinda, Nec sasa itatakiwa kutangaza uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo ndani ya siku 90 kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Lakini katika kile kinachoonekana harakati za kukitwaa kiti hicho, vyama vya CUF, Chadema, NCCR Mageuzi, TLP, UDP, CCM na SAU, jana vililithibitishia gazeti hili kwamba vitasimamisha wagombea wao wa ubunge katika uchaguzi mdogo utakaotangazwa na Nec hivi karibuni.
CUF yataja wagombea wao
CUF kimetoa onyo kwa vyama vya upinzani kuwa ni bora vingeacha kugombea jimbo hilo kwa kuwa tayari chenyewe kimelitwaa.
Katika kuonyesha majigambo, chama hicho kilisema kina nafasi kubwa ya kuchukua ushindi katika jimbo hilo kutokana na mgombea wao, Leopard Mahana, kuombwa na wananchi kugombea tena ubunge baada ya kubwagwa na Rostam kwenye uchaguzi wa mwaka jana.Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, CUF haitafanya kosa la kuliacha jimbo hilo tena.
Alisema hayo muda mfupi baada ya kutoa rambirambi kwa Ubalozi wa Norway nchini kutokana tukio la vifo vya watu 93 vilivyotokana na milipuko ya mabomu nchini humo. “Vyama vya upinzani wasijidanganye kusimamisha mbunge katika jimbo hilo kutokana na chama chetu kuwa na nafasi kubwa ya kushinda kutokana na wananchi wa eneo hilo kumchagua kijana wetu kugombea jimbo hilo,” alitamba Lipumba na kuongeza:
“Katika uchaguzi wa mwaka jana chama chetu ndio pekee kilichosimamisha mgombea kati ya vyama vya upinzani kushindana na Rostam, hivyo vyama vya upinzani kwa sasa vinapaswa kuachia nafasi kama vilivyofanya kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,”alisema Lipumba.
Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, Jimbo la Igunga lillikuwa na wagombea wawili ambao ni Rostam kupitia CCM pamoja na Mahana kupitia CUF.
Chadema waja na Opesheni Chukua Igunga
Kwa upande wake,Chadema kimesema kitaweka mipango yake hadharani hivi karibuni ya namna kilivyojipanga kuingia kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.
Katibu Mkuu wa Chadema hicho, Dk Willibrod Slaa aliliambia Mwananchi jana kuwa chama kimedhamiria kuweka mgombea katika jimbo hilo na hata sasa vijana wako jimboni.“Mikakati ipo,na tutaiweka hadharani baadaye kwa sasa ni mapema mno, lakini vijana wetu wapo kule,”alisema Dk Slaa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, John Heche aliliambia Mwananchi juzi kuwa wanakwenda Igunga kuzindua Opresheni ya Chukua Igunga.“Kama tulivyo na utaratibu wa kuwa na operesheni za kujenga chama ambazo mara nyingi zimejulikana kwa jina la Operesheni Sangara, safari hii katika moja ya mikakati ya kulichukua Jimbo la Igunga, Chadema imeandaa Operesheni Chukua Igunga,”alisema Heche.
Oparesheni hiyo ya siku ilianza juzi Jumapili na inaongozwa na vijana ambapo Mwenyekiti huyo alisema kazi ya kuchukua jimbo imekabidhiwa kwao.
NCCR-Mageuzi yapeleka ujumbe Igunga
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema chama hicho kitasimamisha mgombea katika Jimbo la Igunga na kusisitiza kuwa kwasasa kimetuma timu ya watu sita kwa ajili ya kutizama hali ya kisiasa ilivyo.
“Timu tuliyoituma itakapolejesha majibu ndio tutaweza kutanzaga watakaochuana kuwania nafasi ya kugombea katika jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR,” alisema Ruhuza,
Hata hivyo, Ruhuza alisema kuna dalili za wazi kwamba idadi kubwa ya vyama vya upinzani vitasimamishwa wagombea katika jimbo hilo, huku akionyesha wasiwasi hali hiyo inaweza kuipa CCM mwanya wa kushinda.
“Kuna dalili za wazi kila chama cha upinzani kitataka kuweka mgombea katika jimbo la Igunga. Ni vyema vyama vya upinzani kukubaliana na kusimamisha mgombea anayekubalika ili iwe rahisi kushinda, lakini waking’ang’ania wataishia kugawana kura tu,” alisema Ruhuza.
Sau nao wamo
Mwenyekiti wa Sau, Paul Kyara alithibitisha kuwa chama hicho pia kitaweka mgombea katika jimbo hilo huku akisisitiza kuwa katika uchaguzi huo mdogo jimbo hilo litachukuliwa na wapinzani.
“Tumetuma timu ya wajumbe watatu kwa ajili ya kutizama hali ya kisiasa wilayani Igunga, timu hiyo itarudi wiki hii na majibu kamili, pamoja na hayo mchakato wa kupata mgombea tayari umeshaanza kufanyika,” alisema Kyara.
UDP yavuta pumzi
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo alisita kuzungumzia uchaguzi huo huku akifafanua kwamba ni mapema mno.“Ndio kwanza imetangazwa kuwa jimbo liko wazi…, sasa ndio kila mtu aseme kuwa atasimamisha mgombea, ni mapema sana kuzungumzia suala hilo,” alisema Cheyo kwa ufupi.
CCM bado inavuta pumzi
Kwa upande wake, CCM kimesema bado hakijakaa kujadili namna kitakavyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga.Akizungumza jana Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CCM bado haijakaa vikao kujadili suala hilo.
“Chama chetu hufanya uamuzi wake kwa kupitia katika vikao, hadi sasa sisi hatujakutana kujadili suala hilo, ”alisema Nnauye.Jimbo la Igunga limeachwa wazi kufuatia aliyekuwa Rostam kujuuzulu nyazifa zake zote ndani ya CCM kwa kile kilichodaiwa ni kujivua gamba, ingawa mwenyewe alikataa.
Nec yapokea barua ya Spika
Kwa upande wa NEC, imekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa Rostam baada ya Spika Makinda kuiandikia.Kaimu Mkurugenzi wa Tume hiyo, Sisti Cariah, alisema barua hiyo imewasilishwa jana kutoka bungeni.“Ni kweli leo (jana) tumepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Rostam Aziz,” alisema Cariah
Kwa mujibu wa Cariah, uteuzi unafanyika kuanzia siku ya 20 hadi 50 tangu Spika wa Bunge kupokea barua na kuiarifu Nec.
Imeandikwa na Fidelis Butahe, Hadija Jumanne na Aziza Masoud, Geofrey Nyangóro .

Chanzo: Mwananchi
Wednesday, July 13, 2011
ROSTAM ajiengua CCM...
UTANGULIZI
WAZEE wangu, kwanza kabisa kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukuma kuzungumza nanyi leo, napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kufikia siku hii ambayo inatukutanisha waja wake.
Wazee wangu wa Igunga, baada ya kufanya hivyo napenda pia kutumia fursa hii kuwashukuru ninyi nyote mmoja mmoja na katika umoja wenu kwa kuitikia wito wangu, kijana wenu, niliyewaomba nije nizungumze nanyi siku hii ya leo.
Nafanya hivyo nikitambua vyema kwamba, kama si nyinyi wazee wangu na wengine wengi ambao hatuko nao hapa leo kwa sababu mbalimbali, ambao mmekuwa na imani kubwa nami nisingeweza kufikia hapa nilipofika sasa.
Wazee wangu, waasisi wa taifa letu walitufundisha kutambua na kuheshimu ukweli kwamba; ‘Uongozi ni Dhamana’ dhana ambayo kila ninapokaa na kutafakari huwa inanirejesha nyuma na kukumbuka jinsi nyinyi mlivyokaa katika umoja wenu na kuniteua mimi, miongoni mwa vijana wenu wengi, kuwa mwakilishi wa Jimbo la Igunga tangu mwaka 1994.
Katika kipindi hicho chote cha utumishi wangu, nyinyi wazee wangu mmekuwa mhimili muhimu ambao umeniwezesha kutimiza wajibu wangu kwa bidii kubwa, maarifa na nidhamu ya hali ya juu nikitambua namna ambavyo mmekuwa na imani kubwa juu yangu.
Ari na moyo wa imani, ushirikiano na mshikamano ambao wazee wangu mmekuwa nao kwangu ndiyo ambao kwa kiwango kikubwa umetuwezesha kufanya kazi kwa pamoja, tukishinda changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikilikabili jimbo letu katika kipindi chote ambacho mmeendelea kuniamini kuwa mbunge wenu kwa miaka 18 sasa.
Wakati nikitambua na kuheshimu ukweli kwamba katika kipindi chote cha ubunge wangu mmekuwa na imani kubwa nami na kuniunga mkono kwa dhati, naamini kwamba kwa upande wangu pia nimejitahidi kwa kadiri nilivyoweza, kutimiza matarajio ya wananchi wa Igunga.
Miongoni mwa mafanikio makubwa tuliyoyafikia kupitia ushirikiano wetu na uongozi wa pamoja ni kwamba, mwaka 1994 Igunga ilikuwa ni wilaya ya mwisho kwa maendeleo mkoani Tabora lakini leo ndiyo ya kwanza, taa za barabarani, bima ya afya kwa kila kaya, zahanati kila kijiji na shule nyingi kuliko idadi ya kata zilizomo kwenye wilaya.
Wazee wangu, nayasema haya nikitambua kwamba, kama ilivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini, mafanikio makubwa tuliyoyapata katika nyanja za elimu, afya, makaazi bora na kilimo katika kipindi chote ambacho mmendelea kuniamini kuwa mbunge wenu kwa miaka 18 sasa.

Wazee wangu, nayasema haya nikitambua kwamba, kama ilivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini, mafanikio makubwa tuliyoyapata katika nyanja za elimu, afya, makaazi bora na kilimo katika kipindi hicho chote hayajaweza kumaliza changamoto zote za maendeleo ambazo zinatukabili.
Wazee wangu, ingawa nimekuwa na kawaida ya kukutana na kuzungumza nanyi mara kwa mara, mmoja mmoja na wakati mwingine katika umoja wenu, wito wangu wa leo una makusudi ambayo kwa kiwango kikubwa ni tofauti na yale ambayo tumeyazoea.
Japokuwa ujumbe ninaotaka kuzungumza nanyi wazee wangu, si mgeni sana masikioni mwenu, tofauti ya leo na mikutano yetu mingine iliyopita ni uamuzi ambao nimekusudia kuufanya na ambao nitayatangaza muda mfupi ujao.
YATOKANAYO
Wazee wangu, naamini mmekuwa mkifuatilia kwa karibu hali ya siasa nchini na hususani afya ya kisiasa na matukio mengine ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho mimi ni mwanachama wake na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) nikiuwakilisha Mkoa wetu wa Tabora.
Naamini kwamba katika kufuatilia kwenu mtakuwa mmebaini kuwapo kwa matukio ambayo kwa namna moja au nyingine yamekuwa yakitokea huku yakiligusa jina langu na wakati fulani nafasi yangu kama kiongozi wa chama hicho.
Wazee wangu, nayasema hayo kwa sababu mara kwa mara ninapokutana nanyi nikiwa katika ziara zangu jimboni na wakati mwingine mnapowasiliana nami kwa njia mbalimbali mmekuwa mkionesha kuguswa kushitushwa na kutaka kujua kulikoni kuhusu mambo hayo yanayotokea.
Mimi, kama mnavyonijua nyote, ni mtu muwazi na mkweli. Siku zote nimekuwa mwepesi sana wa kuwaeleza kuhusu kila kinachotokea ili kuwaondoa hofu na wakati huo huo kuwahakikishia kwamba masuala yasiyo na msingi hususani yale yanayogusa siasa za kitaifa hayawezi kutuondoa katika mstari sahihi wa kuwahudumia wananchi wa Igunga, mkiwamo nyinyi wazee wangu ambao mmeniamini na kunituma kuwawakilisha.
Nyinyi wenyewe ni mashahidi wazuri kwamba tangu matukio yanayogusa jina langu yaanze kutokea miezi michache tu baada ya Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikweti kuingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2005, tumekuwa tukiyapuuza na tukaendelea kufanya kazi pamoja kwa bidii.
Bado naamini na nitaendelea kuamini kwamba tulifanya uamuzi sahihi wa kuyapuuza matukio hayo kwani mbali ya kuendelea kutimiza malengo mbalimbali yaliyokuwamo katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya CCM, pia mliendelea kuniamini kwa nafasi yangu ya kuwa mwakilishi wenu bungeni na hata mkaniruhusu nibebe jukumu jingine kubwa la kuwa Mjumbe wa NEC ninayewakilisha mkoa wetu wa kihistoria wa Tabora.
Wazee wangu, nyinyi ndiyo watu mnaolifahamu vyema jimbo letu la Igunga na hakika nyinyi ni sehemu muhimu ya watu wanaojua historia ya kisiasa ya Mkoa wa Tabora kwa miaka mingi hata kabla ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini.
Hakuna shaka hata kidogo kwamba, Tabora ni kitovu hasa cha uasisi wa siasa za vyama vingi hapa nchini. Ni wazi kwamba huwezi ukazungumzia chimbuko la vyama vya upinzani tunavyoviona hapa nchini leo pasipo kugusa mkoa huu ambao umekuwa chimbuko la wanasiasa wenye mizizi hapa na nchini kwa ujumla.
Majina ya wanasiasa wa aina ya wazee wetu, hayati Chifu Said Abdallah Fundikira na Christopher Kassanga Tumbo, Kasela Bantu (Mungu awalaze mahala pema peponi), James Mapalala, Profesa Ibrahim Lipumba na mengi mengine yana mizizi yao katika Mkoa wetu wa Tabora.
Kutokana na ukweli huo basi ni wazi kwamba, nikiwa Mbunge wa Igunga kwa vipindi vinne mfululizo na wakati huo huo nikiwa Mjumbe wa NEC kwa vipindi vitatu mfululizo, moja ya kazi ambazo nimezifanya kwa uaminifu na kwa bidii kubwa huku nikiungwa mkono na kushirikiana nanyi ni ile ya kuhakikisha kwamba mkoa huu pamoja na kuwa kitovu cha upinzani unaendelea kubakia kuwa ngome muhimu ya kisiasa ya CCM.
Si vibaya tukakumbushana kwamba, wakati nachaguliwa kuwa mjumbe wa NEC wa Mkoa mwaka 1997, jimbo moja katika mkoa wetu lilikuwa likishikiliwa na upinzani. Leo hii Tabora ni mkoa pekee miongoni mwa mikoa iliyotuzunguka ambao haukupoteza jimbo hata moja kwenda upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2010. Mafanikio haya tuliyafikia kwa pamoja kutokana na ushirikiano wenu wazee wangu.
Wazee wangu, Waswahili wanasema usione vyaelea, vimeundwa. Kazi ya kuijenga CCM katika mazingira yenye mizizi hasa ya upinzani nikiwa mbunge na hususani M-NEC kutoka Mkoa wa Tabora haijapata kuwa rahisi na itaendelea kuwa ngumu na ambayo mapambano yake ni makali sana.
Wazee wangu, kwa namna ya pekee kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi wazee wangu wa Igunga na wananchi wenzangu wote wa Mkoa wa Tabora kwa kushikamana na kuifanya kazi hiyo kwa bidii, uaminifu na mafanikio makubwa.
Matunda ya kazi hiyo kubwa yanaonekana. Pamoja na kuwa kitovu cha kihistoria cha siasa za upinzani, Tabora ndiyo mkoa pekee katika eneo hili ambao unaongozwa na wabunge wote kutoka CCM baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na hata kabla ya hapo.Kwa sababu hiyo basi, wazee wangu, sote katika umoja wetu ukiacha mafanikio makubwa tuliyopata katika jimbo na Wilaya yetu ya Igunga, tunayo mambo mengine ya msingi ya kujivunia. Kwa moyo wa dhati na kwa unyenyekevu mkubwa napenda kuwapongeza kwa namna mlivyojitoa kukipigania na kukitetea chama chetu kwa ari na nguvu ya kipekee.

KUJIVUA GAMBA
Wazee wangu, chama chetu chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kimeamua kwa kauli na nia moja kujitathmini na kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo yenye lengo la kukiwezesha kiendelee kubakia chama kinachoaminiwa na kuungwa mkono na Watanzania walio wengi.Dhamira ya mwelekeo huo wa kufanya mabadiliko ya ndani ya chama chetu ilitangazwa rasmi na Mwenyekiti wetu Rais Kikwete wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, mjini Dodoma.Katika hotuba yake hiyo, Rais Kikwete aliyafananisha mabadiliko hayo na tabia ya kawaida na ya asili ya nyoka na wanyama wengine kadhaa ya ‘Kujivua Gamba’.
Wazee wangu hatua ya kwanza ya utekelezaji wa azimio hilo na mwelekeo huo sahihi ilifanyika mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya CCM ambacho mimi nilikuwa mjumbe wake.Wakati wa kikao hicho, wajumbe wote wa Kamati Kuu na wale wa Sekretarieti ya chama chetu wa wakati huo kwa kauli moja tulikubaliana kujiuzulu, lengo likiwa ni kumpa Mwenyekiti wetu fursa nzuri ya kufanya mabadiliko ya uongozi yatakayotoa nafasi ya kupata mwelekeo mpya wa Chama.
Wazee wangu, tulifanya hivyo tukionesha kuunga mkono kwa asilimia 100 kile ambacho bado naendelea kuamini kuwa ni mawazo sahihi na yenye mwelekeo thabiti ya Mwenyekiti wetu ambayo kwa kiwango kikubwa yalikuwa yakiakisi matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa urais, ubunge na udiwani wa Oktoba mwaka jana.Niliseme kwa maneno machache tu hili. Ingawa ni kweli kwamba Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana umekirudisha madarakani chama chetu kwa kukipa ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani kwa Tanzania Bara na Zanzibar, kiwango cha ushindi tulichopata kimeonyesha waziwazi dalili za wananchi kupunguza imani yao kwetu kuilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2005.Tungekuwa ni chama cha siasa cha ovyo iwapo tungepuuza kupungua kwa kura za rais kutoka zaidi ya asilimia 80 tulizopata mwaka 2005 hadi kufikia aislimia 61 mwaka jana kiwango ambacho ni pungufu kwa asilimia 20 ya kura katika kipindi cha miaka mitano tu, hasa ikizingatia ukweli kwamba mgombea urais ni mtu yule yule.Tungekuwa ni chama cha siasa kilichokosa umakini iwapo tungekaa pasipo kuchukua hatua zozote za kujiimarisha baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu kuonesha wazi kukua kwa upinzani ambao umeongeza idadi ya wabunge na madiwani katika pande zote mbili za muungano.Matokeo hayo ya uchaguzi ambayo hapana shaka yamekitikisa chama chetu yalitukumbusha wasia ambao tuliachiwa na Baba wa Taifa aliyesema; ‘Bila ya CCM Madhubuti Nchi Yetu Itayumba’.
Wazee wangu, kwa sababu ya kutambua ukweli kwamba hakuna haki isiyo na wajibu kama nilivyosema awali, mimi na wenzangu tuliokuwa katika Kamati Kuu tuliona ulazima, haja na umuhimu wa kukubali kwa kauli moja wito wa kututaka tujiuzulu ikiwa ni hatua moja ya kujipanga na kukijenga upya chama chetu.
KUJIVUA GAMBA KWAPOTOSHWA
Wazee wangu, kilichotokea baada ya kujiuzulu kwetu kila aliye ndani na nje ya chama chetu amekisikia na anakifahamu. Chama kilipata safu mpya ya uongozi iliyotokana na kuundwa kwa Sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wetu mpya, Mhe. Wilson Mukama, na Kamati Kuu iliyokuwa na sura tofauti na ile ya awali.Wakati tukitafakari na kuangalia mustakabali mpya wa kisiasa ndani ya chama chetu, ghafla yalianza kutokea mambo ambayo chokochoko zake zilianza kusikika tangu tukiwa ndani ya Kamati Kuu ambayo ilijiuzulu baadaye.Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kilichagua wajumbe wapya wa Kamati Kuu na kuidhinisha uundwaji wa Sekretarieti mpya, dhana ya kujivua gamba ambayo naamini Mwenyekiti wetu aliianzisha kwa nia njema ilianza kuenezwa ikichukua tafsiri na mwelekeo tofauti na ule wa awali.Wajumbe wawili wa Sekretarieti, Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Mhe. John Chiligati, na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Nape Nnauye, walisikika wakitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuwa imefikia uamuzi wa kuwapa siku tisini wale walioitwa watuhumiwa wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi ndani ya chama kujitoa katika nafasi zao za uongozi vinginevyo watafukuzwa na chama.
Wazee wangu, baada ya kushinikizwa sana na vyombo vya habari wawataje kwa majina wanasiasa waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi ambao ni wajumbe wa NEC na ambao wanapaswa kujiuzulu nyadhifa zao, wajumbe hao wa Sekretarieti walikwenda mbele zaidi.Baada ya awali kuwaeleza waandishi wa habari kwamba majina ya watuhumiwa hao yalikuwa yakifahamika kutokana na kuhusishwa katika kashfa tofauti kama zile za Richmond, EPA na ununuzi wa rada, mwishoni viongozi hao walikaririwa wakiyataja majina ya wanasiasa watatu kuwa ndiyo ambao walikuwa wakilengwa na maamuzi hayo.
Wazee wangu, nilishangazwa na kushitushwa na namna porojo na fitina za kisiasa zilivyofinyangwa kwa mara nyingine tena baada ya kusikia jina la mbunge wenu ambaye ni mimi, likitajwa kuwa miongoni mwa yale matatu ya viongozi waliokuwa wakitakiwa eti kupima wenyewe na kisha kuchukua uamuzi wa kujiuzulu nafasi zao za uongozi ndani ya NEC katika kipindi cha siku tisini.Niliseme hili mapema. Mshangao na mshituko wangu haukusababishwa na kutajwa kwa jina langu, la hasha, bali namna uamuzi halisi wa NEC na hususani dhana nzima ya ‘kujivua gamba’ ilivyoweza kupindishwa na wajanja wachache na kisha kuendeshwa kwa maslahi binafsi ya kikundi fulani cha watu.
Pili, nilishangazwa na kushitushwa na hatua ya viongozi wa chama changu ambacho nimekitumikia kwa bidii na uaminifu mkubwa kufanya juhudi kubwa hata kukivisha kikao kitukufu cha NEC uamuzi ambao msingi wa hoja zake ni vita vya kimakundi ya kisiasa yaliyo ndani ya CCM kwa upande mmoja na propaganda za vyama vya siasa vya upinzani na vyombo vya habari kwa upande mwingine.Tatu, nilishangazwa na kushitushwa na ujasiri ambao umekuwa ukioneshwa na baadhi ya viongozi wetu wapya wa Sekretarieti wanaolitaja jina langu na kulihusisha na kile wanachokiita ufisadi ambao hata ukweli wa kimazingira na kihistoria ukiachilia mbali ushahidi wa wazi umeshathibitisha kwamba ni porojo za kisiasa zilizotokana na makovu na matarajio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na ule ujao wa 2015.
Wazee wangu, nyinyi ni mashahidi kwamba, mbali ya mimi mwenyewe kujitokeza kupitia vyombo vya habari na kueleza wazi kwamba sijapata kujihusisha katika vitendo vyovyote vya ukiukwaji wa maadili ya uongozi au vya rushwa, hakuna ushahidi wowote uliotolewa unaonihusisha na kashfa yoyote miongoni mwa zile zilizotajwa.Wazee wangu, ni wazi kwamba kama chama chenye siasa chenye dhamana ya kuwaoongoza Watanzania kutoka katika lindi la ufukara, maradhi, matatizo ya makaazi na mengineyo siku zote tunapaswa kuwa makini katika kuhakikisha kwamba changamoto za kuwaongoza na kuwakomboa wananchi waliotupa dhamana hazitikiswi na mawimbi ya matakwa ya nyakati ama ya vyombo vya habari au wapinzani wetu wa kisiasa walio nje ya CCM.Ni kwa sababu ya kulitambua hilo na hasa kuyatambua madhara yanayoweza kukipata chama chetu na nchi yetu iwapo tutaendekeza siasa za kupakana matope pasipo na sababu za msingi, kuchafuana kusikokoma na kulipizana kisasi ndiyo maana nimeona nitumie fursa hii kuzungumza nanyi wazee wangu ili kuweka kumbukumbu sahihi.
MAAMUZI YANGU
Wazee wangu, nimetafakari sana na kimsingi nimefikia hatua ya kupima yale ambayo yamekuwa yakisemwa na kuandikwa juu yangu na ambayo kwa mtazamo wangu unaoungwa mkono na wanafamilia yangu, marafiki zangu na washirika wangu wa kibiashara walio ndani na nje ya nchi, naona umefika wakati muafaka wa kuchukua hatua.Kwa sababu ya kutambua uzito wa hatua ninazokusudia kuzichukua, niliona halitakuwa jambo la hekima hata kidogo iwapo ningefanya hivyo pahala pengine popote bali hapa Igunga mbele ya nyie wazee wangu.Baada ya kukaa na wanafamilia yangu, marafiki na washirika wangu wa kibiashara niliona halitakuwa jambo la busara hata kidogo kuendelea kuvutana na viongozi wa chama changu na wanachama wenzangu wa CCM katika mambo ambayo yanaweza kumalizwa kwa njia muafaka.
Wazee wangu, sina budi niwaeleze kwamba, mbali ya athari za kisiasa na kifamilia, vita vya ovyo vya kisiasa kama hivi tunavyoviendesha na kuviendeleza ndani ya CCM na ndani ya nchi yetu huwa vina athari kubwa katika ulimwengu wa kibiashara. Athari kama hizo za kibiashara huingia ndani zaidi kuliko vichwa vya habari vya magazeti vinavyolenga kuchafuana, na athari hizo huwa kubwa zaidi kwa mtu kama mimi kwa sababu tofauti na wengine wengi hapa nchini, mimi ni mfanyabiashara wa kimataifa.
Katika ulimwengu wa kibiashara wa leo, vita hivi ambavyo vinaweza kuonekana kuwa ni vidogo tu vyenye malengo ya kuchafuana kisiasa, vinakuwa na athari kubwa katika uhusiano wa kibiashara kuliko hata wale wasioelewa wanavyoweza kukadiria. Ndiyo maana nimeona ni afadhali sasa niwape nafasi wale wanaoendesha siasa hizi uchwara na zisizo na tija waendelee na siasa zao hizo ambazo kwa bahati mbaya kwao, mimi sina muda nazo na siwezi kuwa sehemu yake. Na mimi kwa upande wangu niendelee na maisha yangu.
Kutokana na ukweli huo na sababu zote hizo basi, kwa moyo wa dhati na kwa nia thabiti, hatua ya kwanza niliyoiona kuwa ninapaswa kuichukua ilikuwa ni hii ya kuitikia wito unaotokana na msukumo wa ndani ya nafsi yangu wa kuamua kukomesha kabisa malumbano na mivutano isiyo na manufaa kwangu binafsi, kwa viongozi wa chama changu na chama chenyewe.Msukumo huo si mwingine bali ni ule wa kuamua kuachia nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama, nikianzia na ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nikiuwakilisha Mkoa wa Tabora na hii ya ubunge wa Igunga ambazo kama si kwa baraka za chama changu nisingelikuwa nazo.
Napenda kuliweka hili sawa sawa. Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara (gutter politics) na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu.
Aidha, nimefikia uamuzi huo lengo likiwa ni kuwajengea heshima na imani machoni mwa wanachama na wananchi wengine, viongozi wangu ambao naamini baada ya mimi kujitoa watapata fursa ya kutafakari upya changamoto nyingine mbadala zinazowakabili ambazo msingi wake ni dhamana kubwa walizo nazo za kukiongoza chama chetu na nchi yetu kupitia Serikali yake.
Wakati nachukua uamuzi huu, natambua vyema kwamba, watatokea watu ndani ya chama chetu na nje ambao watafanya kila juhudi kupotosha au kupindisha ukweli kuhusu hatima yangu ya kisiasa baada ya kujiweka kando na kujipa mimi mwenyewe na chama changu fursa ya kutafakari kwa kina majaaliwa yangu na ya nchi yangu katika siku zijazo.Nafanya hivyo nikiwa na imani thabiti kwamba, uamuzi wangu huu, hususani ule wa kuachia nafasi yangu ya ubunge, yatakipa fursa nyingine CCM ya kuendelea kuliongoza jimbo letu la Igunga katika kipindi cha miaka minne ijayo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Kwa upande mwingine, uamuzi wangu huu naona ni fursa kwa viongozi wa Chama changu cha CCM kutafakari na kuamua njia wanayoiona wao ni sahihi kuichukua kwa hatima na mustakabali wa chama chetu na ambayo wanaamini itakipa nguvu mpya ya kisiasa dhidi ya vyama vya upinzani.Sambamba na hilo, ninayo imani thabiti kwamba, uamuzi wangu wa kubakia kuwa mwanachama wa kawaida na mtiifu wa CCM utakuwa chachu kwa chama changu na kwa Serikali yake kuwatumikia wananchi kwa Ari Zaidi, Kasi Zaidi na Nguvu Zaidi.Mwisho kabisa, nikimalizia naomba nitumie fursa hii kutoa heshima za pekee kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa aliyoifanyia na anayoendelea kuifanyia nchi yetu. Amefanya mengi na makubwa kuiendeleza nchi yetu na watu wake kuliko inavyothaminiwa na kufahamika. Kazi yake kubwa inashindwa kuthaminiwa na kufahamika kutokana na siasa chafu tunazoziendesha Tanzania. Wasia wangu kwa wanasiasa wenzangu, waandishi wa habari na Watanzania wenzangu kwa ujumla ni kuwa tunahitaji kuisaidia nchi yetu kwa kufanya siasa zenye mwelekeo wa kujenga ambazo ndiyo hasa zinapaswa kuwa siasa kwa maana halisi ya neno hilo.
Wazee wangu, baada ya maelezo hayo, nawashukuru sana kwa kunisikiliza na kunielewa.
Ahsanteni sana.

Mwisho…
Tuesday, July 12, 2011
COCACOLA Kwanza Dar wagoma.
Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha soda cha Coca Cola Kwanza, kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakiwa katika mgomo wao leo asubuhi. Wafanyakazi hao waligoma wakishinikiza uongozi wa Kiwanda hicho uwaongezee mishahara.
Baadhi ya wafanyakazi wakiongea na waandishi wa habari.
Kiongozi wa TUICO alifika kuwatuliza wafanyakazi hao na kuahidi kuzungumza naMenejimenti ya Kiwanda hicho. Mpaka kamera ya mjengwablog inaondoka eneo la Kiwanda hicho majira ya saa sita mchana, mgomo ulikuwa unaendelea na Uongozi wa kiwanda hicho ulikataa kuzungumza chochote na waandishi wa habari.
BEST WISHES TO ALL WHOARE STARTING THEIR EXAMS
NAWATAKIA mitihani myema wale wote wanaotaraji kuanza mitihani yao ya mwisho wa mwaka vyuoni.
REST in Peace Dear Brother.
Marehem John Mbwilo akiwa chuoni SUA Morogoro.
Akiwa amepozi nyumbani kwao Morogoro enzi za uhai wake.
Marehemu John Mbwilo enzi za uhai wake.
Tulipokuwa tunasoma Olduvai, sijaweza kutambua mahali alipo katika picha hii (Japo yupo) lakini nikimwona nitawaambia. Pichani ni wanafunzi wenzake tuliosoma wote Olduvai 2003-2006 mimi nikiwemo.
KWA huzuni na masikitiko makubwa nasikitika kumpoteza ndugu yetu, kaka yetu, rafiki yetu na mtu wetu wa karibu John Mbwilo. Tulikuwa na John miaka michache iliyopita 2007 wakati mimi ninarudia masomo yangu ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Majengo Moshi yeye alikuwa kidato cha tano Old Moshi Sekondari. Alikuwa akisoma na classmate wetu mwingine Bonaventure Kway na kwa bahati mbaya nilikuwa nikionana naye mara chache sana kwani Bonny nilikuwa naonana naye kanisani wakati Mbwilo yeye ni Mlitheri hivyo kuonana kanisani ilikuwa ni vigumu maana mimi ni Mkatoliki. pia kutokana na masomo aliyosoma, yeye alisoma PCB wakati Bonny alisoma PCM. Kama ujuavyo masomo hayo ya sayansi humweka mtu bize sana.
Baada ya kumaliza kidato cha sita, John alipangwas kusoma SUA Morogoro. hiuvyo wakati mimi nikiwa mwaka wa Kwanza Tumaini Iringa, yeye alikuwa mwaka wa pili SUA Morogoro. Kwa maisha tuliyoishi na John Mbwilo wakati akijiita JM kule Olduvai yalikuwa ya furaha na tuliishi naye vizuri. Nakiumbuka siku moja alitupeleka kwa bibi yake maeneo ya hukohuko chuoni, tukaenda kusalimia wazazi wake walikuja kumsalimia. We enjoyed being with him. Sote tumuombee kwa Mungu ili ampe faraja na Raha ya milele.
APUMZIKE KWA AMANI AMINA!
Wednesday, July 06, 2011
TUMAINI UNIVERSITY, IRINGA UNIVERSITY COLLEGE
Second Semester Examinations(Final Draft) BACD First Year_GRP 1 (Wk 1)
08:30 11:30 11:35 14:00 14:00 17:00
14:00-17:00, Wk 1, 18/07/2011
Information and Communication Technology II
CAFE HALL
BACD First Year_GRP 1 [80]
Mon
18 Jul
14:00-17:00, Wk 1, 19/07/2011
Principles of Management
MULTIPURPOSE
BACD First Year_GRP 1 [80]
Tue
19 Jul
Wed
20
08:30-11:30, Wk 1, 21/07/2011
Communication Skill II
New Lecture Theatre
BACD First Year_GRP 1 [80]
Thu
21 Jul
14:00-17:00, Wk 1, 22/07/2011
Child Care, Development and Safe Motherhood
NE 1
BACD First Year_GRP 1 [80]
Friday
22 Jul
Page 1, published 1-Jul-11, by IUCO (Sokoine University of Agriculture) - CELCAT Timetabling

Second Semester Examinations(Final Draft) BACD First Year_GRP 1 (Wk 2)
08:30 11:30 11:35 14:00 14:00 17:00
08:30-11:30, Wk 2, 25/07/2011
Social Change and Development
NE 1
BACD First Year_GRP 1 [80]
Mon
25 Jul
Tue
26
08:30-11:30, Wk 2, 27/07/2011
Social Psychology
NE 1
BACD First Year_GRP 1 [80]
Wed
27 Jul
08:30-11:30, Wk 2, 28/07/2011
Introduction to Leadership
New Lecture Theatre
BACD First Year_GRP 1 [80]
Thu
28 Jul
08:30-11:30, Wk 2, 29/07/2011
Gender and Development
NE 1
BACD First Year_GRP 1 [80]
Friday
29 Jul
Page 2, published 1-Jul-11, by IUCO (Sokoine University of Agriculture) - CELCAT Timetabling

Tuesday, July 05, 2011
KUJIFARIJI mwenyewe kunakusaidia?
TUNAPOTAFUTA faraja, tunajichanganya na watu wanaotimiza haiba ya ubinadamu wetu na kujihisi kuwa hatuhitaji kujumuika na kitu kingine chochote zaidi yao na kwa kujiamini kabisa tunawaita wao kuwa ni "marafiki". Kuna mamaia ya watu tunaowaita marafiki kwa kuwa tu majina yao na namba zao vipo kwenye simu zetu za mikononi na kwa kuwa hutusaidia na kutufanikishia mambo fulani fulani.
Tunakuwa mabingwa wa mahusiano ya usiku mmoja ambayo hutusaidia kugundua haiba zetu na si zaidi ya hapo. Tunajikuta tukipoteza muda mwingi tukijishughulisha na maisha ya watu wengine au kushughulika na uhusiano wa muda mfupi na watu wengine huku tukisahau kwamba maisha tunayoishi ni yetu wenyewe.
Hii haiondoi ukweli kwamba watu wengine wanaathiri maisha yetu, lakini hatimaye sisi (mimi na wewe) ndio wadhibiti wa maisha yetu wenywe.
TAFAKARI......!!!! CHUKUA HATUA.....!!!!
NILPOKUWA Mbeya kwa ziara ya kimasomo mapema mwaka huu.
HAPA ndipo tulipolala maeneo ya Uyole, Asubuhi Mbeya kuna baridi acha mchezo.
HAPA ni Chuo cha Kilimo MATI-Uyole, tulipoenda kutembelea kupata ujuzi kidogo wa Extension education. Tulifaidi lakini.
TUKAONELEA si vyema tukawa peke yetu, hapa tukamchukua Mhadhiri (Leacturer) Mama Msomba tupate nae picha ya pamoja. Tunamshukuru Mungu tulirudi salama usalimini.
UJUMBE wangu kwa Adella.
Mpendwa Adella,
USIWE na mapapara, maisha kuparamia,
Ujiweke imara, ukubali kuvumilia,
Hata kupata harara, uwe radhi kuvumilia,
Ndoa kweli msalaba, yataka uvumilivu.
ADELLA, bahari haivukwi kwa kuogelea.
Best of luck Mama. You are grown up enough now,
an expected mother. Tangulia sisi twaja. Msalimie shemeji.
CLASSMATE wangu aliukataa ukapera mwezi uliopita. Ni Adella Peter.
Ilikuwa ni furaha siku hiyo Adella ndani ya Shela
Hapa akiwa na mwanamajengo Raya Said akimpa kampani mtoto A.D. Dah!!! It was very very fantastic!! CONGRATULATION ADELLA!!!
Saturday, July 02, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)